Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 8:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Akaja mwenye ukoma akamsujudu, akinena, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Basi, akaja mtu mmoja mwenye ukoma, akamsujudia na kusema, “Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Basi, akaja mtu mmoja mwenye ukoma, akamsujudia na kusema, “Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Basi, akaja mtu mmoja mwenye ukoma, akamsujudia na kusema, “Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Mtu mmoja mwenye ukoma akaja na kupiga magoti mbele yake, akasema, “Bwana, ukitaka, unaweza kunitakasa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Mtu mmoja mwenye ukoma akaja na kupiga magoti mbele yake, akasema, “Bwana, kama ukitaka, unaweza kunitakasa.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 8:2
37 Marejeleo ya Msalaba  

Ponyeni wagonjwa, takaseni wenye ukoma, fufueni wafu, fukuzeni pepo; mmepata burre, toeni burre.


Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutokuamini kwao.


Nao waliokuwa ndani ya chombo wakamwendea, wakamsujudia, wakinena, Hakika wewe u Mwana wa Mungu.


Nae akaja akamsujudia, akinena. Bwana, nisaidie.


Bassi yule mtumishi akaanguka, akamsujudia akinena, Bwana, niwie kwa saburi, nami nitakulipa vyote pia.


Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mama yake, wakaanguka wakasujudu; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tumi, dhahabu, uvumba, na manemane.


Ndipo mama ya wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akimsujudia, akimwomba neno.


Nae Yesu, alipokuwa Bethania katika nyumba ya Simon mwenye ukoma,


Nao walipomwona, wakamsujudia; lakini wengine waliona shaka.


Nao walipokuwa wakienda kuwapasha wanafunzi wake khabari, Yesu akakutana nao, akinena, Salam! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia.


Hizi zote nitakupa, ukianguka kunisujudia.


ALIPOSHUKA mlimani, makutano mengi walimfuata.


Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakinena, Bwana, tuokoe tunaangamia.


Alipokuwa akiwaambia haya, yuaja jumbe mmoja, akamsujudia, akinena, Binti yangu udio kwanza afe: lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, uae atapona.


Tena palikuwa wengi wenye ukoma katika Israeli zamani za nabii Elisha: wala hapana aliyetakasika illa Naaman, mtu wa Sham.


Akasema, Naamini, Bwana; akamsujudia.


Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijala kamwe kitu kilicho kichafu au najis.


Petro alipokuwa akiingia, Kornelio akatoka amlaki akamwangukia miguu, akamsujudia.


na hivyo siri za moyo wake huwa wazi; na hivyo, akianguka kifudifudi, atamwabudu Mungu, akikiri ya kuwa Mungu yu kati yenu hila shaka.


Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo