Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 8:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Ilipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo: akawafukuza pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi,

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Ilipokuwa jioni, walimletea watu wengi waliokuwa wamepagawa na pepo; naye, kwa kusema neno tu, akawafukuza hao pepo. Aliwaponya pia watu wote waliokuwa wagonjwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Ilipokuwa jioni, walimletea watu wengi waliokuwa wamepagawa na pepo; naye, kwa kusema neno tu, akawafukuza hao pepo. Aliwaponya pia watu wote waliokuwa wagonjwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Ilipokuwa jioni, walimletea watu wengi waliokuwa wamepagawa na pepo; naye, kwa kusema neno tu, akawafukuza hao pepo. Aliwaponya pia watu wote waliokuwa wagonjwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuwaponya wagonjwa wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuwaponya wagonjwa wote.

Tazama sura Nakili

Mathayo 8:16
17 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu na bubu; akamponya, hatta yule kipofu na bubu akasema na kuona.

Yesu akatoka, akaona makutano mengi, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao.

Akamgusa mkono wake, homa ikamwacha; nae akaondoka, akawatumikia.

Wachungaji wakakimbia, wakaenda zao mjini, wakayakhubiri yote, na mambo ya wenye pepo pia.

Wakamletea mgonjwa wa kupooza, amelala kitandani: na Yesu, akiona imani yao, akamwambia yule mgonjwa wa kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanaugu; umeondolewa dhambi zako.

Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wane.

Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu.

Nae Yesu akiona ya kuwa makutano yanakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu ua kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke, wala usimwingie tena.

Bassi Yesu alipomwona, akamwita, akamwambia, Ee mwanamke, umefunguliwa udhaifu wako.

Hatta jua lilipokuwa likichwa watu wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbali mbali wakawaleta kwake: nae akaweka mikono yake juu ya killa mmoja, akawaponya.

Pepo wakawatoka wengi wakipaaza sauti zao wakisema, Wewe u Kristo, Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walijua ya kuwa yeye ndiye Kristo.

hatta katika njia kuu hutoa nje wagonjwa, huwaweka juu ya mifarashi na vitanda, illi, Petro akija, kivuli chake tu kimtie kivuli mmojawapo wao.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo