Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 8:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 Yesu aliposikia haya, akastaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa kama hii, hatta katika Israeli.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia watu waliokuwa wanamfuata, “Kweli nawaambieni, sijapata kumwona mtu yeyote katika Israeli mwenye imani kama hii.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia watu waliokuwa wanamfuata, “Kweli nawaambieni, sijapata kumwona mtu yeyote katika Israeli mwenye imani kama hii.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia watu waliokuwa wanamfuata, “Kweli nawaambieni, sijapata kumwona mtu yeyote katika Israeli mwenye imani kama hii.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Isa aliposikia maneno haya, alishangaa, akawaambia wale waliomfuata, “Amin, nawaambia, hata katika Israeli sijapata kuona yeyote mwenye imani kubwa namna hii.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Isa aliposikia maneno haya, alishangaa, akawaambia wale waliomfuata, “Amin, nawaambia, hata katika Israeli sijapata kuona yeyote mwenye imani kubwa namna hii.

Tazama sura Nakili

Mathayo 8:10
9 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Ee mwanamke, imani yako kubwa; pata utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.

Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magbaribi, wataketi pamoja na Ibrabimu, na Isaak, na Yakob katika ufalme wa mbinguni;

Maana na mimi ni mtu chini ya mamlaka, nina askari chini yangu: nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; au mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.

Akastaajahu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Akazungukazunguka katika vile vijiji, akifundisha.

Alipoona imani yao, akamwambia, Ee mtu, dhambi zako zimeondolewa.

Akamwambia yule mwanamke, Imani yako imekuokoa; enenda zako kwa amani.

Yesu aliposikia haya akamstaajabia akawageukia makutano waliokuwa wakimfuata, akisema, Nawaambieni, Hatta katika Israeli sikuona imani nyingi namna hii.

Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Si hawa wote wasemao Wagalilaya?

Tufuate:

Matangazo

Matangazo