Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 7:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Bassi killa asikiae haya maneno yangu, na kuyafanya, nitamfananisha na mtu mwenye akili aliyejenga nyumba vake juu ya mwamba:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 “Kwa hiyo, kila mtu anayeyasikia maneno yangu na kuyazingatia, anafanana na mtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 “Kwa hiyo, kila mtu anayeyasikia maneno yangu na kuyazingatia, anafanana na mtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 “Kwa hiyo, kila mtu anayeyasikia maneno yangu na kuyazingatia, anafanana na mtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 “Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 “Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba.

Tazama sura Nakili




Mathayo 7:24
41 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana ye yote atakaeyafanya mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.


Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na jun ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; na milango ya kuzimu haitalishinda.


Nani bassi aliye mtumishi yule amini mwenye haki, ambae bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape chakula kwa saa yake?


Watano wao walikuwa wenye busara, ua watauo wapumbavu.


bali wale wenye busara walitwaa na mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.


Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakinena, Labuda hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia kwenda kwao wauzao, mkanunue wenyewe.


mvua ikanya, maji mengi yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa katika mwamba.


Na killa asikiae haya maneno yangu, asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, alivejenga nyumba yake katika mchanga;


Lakini yeye akasema, Bali afadhali wa kheri wenye kulisikia neno la Mungu na kulishika.


Mkiyajua hayo, m kheri mkiyatenda.


Mkinipenda mtazishika amri zangu.


Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu, na kukaa katika pendo lake.


Ninyi m rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.


Kwa sababu sio waisikiao torati walio wenye haki mbele ya Mungu, bali ni wale waitendao torati watakaohesabiwa kuwa wenye haki.


Na hivi twajua ya kuwa tumemjua, ikiwa tunashika amri zake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo