Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 7:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kufukuza pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Wengi wataniambia siku ile ya hukumu: ‘Bwana, Bwana! Kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi’.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Wengi wataniambia siku ile ya hukumu: ‘Bwana, Bwana! Kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi’.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Wengi wataniambia siku ile ya hukumu: ‘Bwana, Bwana! Kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi’.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Wengi wataniambia siku ile, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo wachafu na kufanya miujiza mingi?’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Wengi wataniambia siku ile, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo wachafu na kufanya miujiza mingi?’

Tazama sura Nakili

Mathayo 7:22
23 Marejeleo ya Msalaba  

Amin, nawaambieni, Itakuwa rakhisi inchi ya Sodoma na Gomora istahimili adhabu yao siku ya hukumu, kuliko mji ule.

Na khabari ya siku ile na saa ile hakuna ajuae, hatta malaika walio mbinguni, illa, Baba yangu peke yake.

Khalafu wakaja na wale wanawali wengine, wakinena, Bwana, Bwana, utufungulie.

Siye killa mtu aniambiae, Bwana, Bwana, atakaeingia katika ufalme wa mbinguni; hali yeye afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

Nawaambieni, itakuwa rakhisi Sodoma istahimili adhabu yake siku ile kuliko mji ule.

Na hili hakusema kwa nafsi yake, hali kwa kuwa alikuwa kuhani mkuu mwaka ule alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa lile;

Bali ninyi, ndugu, hamwi katika giza, siku ile iwapale kama mwizi.

atakapokuja illi kutukuzwa katika watakatifu wake, na kuajabiwa katika wote waaminio (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu), katika siku ile.

Kwa sababu hiyo nimepata mateso haya, wala sitahayariki: maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki kwamba aweza kukilinda kile nilichakiweka amana kwake hatta siku ile.

Bwana na ampe kuona rehema kwa Bwana siku ile. Na jinsi alivyonikhudumia katika Efeso, wewe wajua sana.

baada ya haya nimewekewa taji ya baki, ambayo Bwana mhukumu wa haki atanipa katika siku ile: wala si mimi tu, bali watu wote pia waliopenda kutokea kwake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo