Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 7:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Kama ninyi, bassi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! si zaidi Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wamwombao?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Kama basi nyinyi, ingawa ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: Atawapa mema wale wanaomwomba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Kama basi nyinyi, ingawa ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: Atawapa mema wale wanaomwomba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Kama basi nyinyi, ingawa ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: atawapa mema wale wanaomwomba.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Ikiwa ninyi basi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?

Tazama sura Nakili




Mathayo 7:11
35 Marejeleo ya Msalaba  

Wala msimwite mtu baba yenu duniani: maana Baba yeuu yu mmoja, aliye mbinguni.


Au akiomba samaki, atampa nyoka?


Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hatta akampeleka Mwana wake wa pekee, illi mtu aliye yote amwaminiye asipotee, bali apate uzima wa milele.


Twajua ya kuwa mambo yote yasemwayo na torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, illi killa kinywa kifumbwe, ulimwengu wote ukapasiwe na hukumu ya Mungu:


Ni nini bassi? Tu bora kuliko wengine? Hatta kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba wote pia wa chini ya dhambi;


Yeye asiyemwachilia Mwana wake yeye, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukarimia na vitu vyote pamoja nae?


Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi waaminio wapewe ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.


Killa kutoa kwenia, na killa kitolewacho kilicho kamili, chatoka juu, chashuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.


FAHAMUNI, ni pendo la nanma gani alilotupa Baba, kuitwa wana wa Mungu. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.


Hili ndilo pendo, si kwamba sisi twalimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akampeleka Mwana wake kuwa kipatanislio kwa dhambi zetu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo