Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 6:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Bassi ninyi salini hivi; Baba yetu nliye mbinguni, jina lako takatifu litukuzwe,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Basi, hivi ndivyo mnavyopaswa kusali: ‘Baba yetu uliye mbinguni: Jina lako litukuzwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Basi, hivi ndivyo mnavyopaswa kusali: ‘Baba yetu uliye mbinguni: Jina lako litukuzwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Basi, hivi ndivyo mnavyopaswa kusali: ‘Baba yetu uliye mbinguni: Jina lako litukuzwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 “Hivi ndivyo mnavyopaswa kuomba: “ ‘Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 “Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba: “ ‘Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.

Tazama sura Nakili




Mathayo 6:9
43 Marejeleo ya Msalaba  

Videge viwili haviuzwi kwa pesa moja? Na hatta mmoja haanguki chini asijiojua Baba yemi:


Wala msimwite mtu baba yenu duniani: maana Baba yeuu yu mmoja, aliye mbinguni.


Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu leo nzao huu wa mzabibu, hatta siku ile nitakapounywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.


Akaenda tena marra ya pili, akaomba, akinena, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kinipitie nisipokinywa, bassi, mapenzi yako yafanyike.


Vivi hivi nuru yenu iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wakamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.


Bassi mwe ninyi wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.


Kwa kuwa wako ni ufalme, na nguvu, na utukufu, hatta milele. Amin. Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe nanyi.


Bali wewe usalipo, ingia chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele ya Baba yako aliye kwa siri: na Baba yako aonae kwa siri atakujazi kwa dhahiri.


Kama ninyi, bassi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! si zaidi Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wamwombao?


Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu, nitamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu, na mbele yako: sistahili kuitwa mwana wako baada ya hayo:


Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili baada ya hayo kuitwa mwana wako.


Utukufu una Mungu palipo juu, Na katika inchi amani, kwa watu aliowaridhia.


Yesu akamwambia, Usiniguse; kwa maana sijapaa kwa Baba yangu. Lakini enenda kwa ndugu zangu, ukawaambie, Ninapaa kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu.


kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu: Neema iwe kwenu na imani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwaua Yesu Kristo.


Kwa kuwa hamkupokea roho ya utumwa uletao khofu, hali mlipokea roho ya kufanywa waua, kwa hiyo twalia, Abba, Baba.


PAOLO, mtume (si mtume wa wana Adamu, wala hakutumwa na mwana Adamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua),


Na kwa kuwa ninyi ni wana, Mungu alimtuma Roho ya Mwana wake mioyoni mwenu, aliaye, Abba, Baba.


ambae yeye peke yake hapatikani na mauti, akaae katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hapana mwana Adamu aliyemwona, wala awezae kumwona, ndiye mwenye heshima na uweza milele. Amin.


Na ikiwa mnamwita Baba yeye ahukumuye killa mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa khofu kafika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni;


Umestahili, Bwana, Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na nweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, vikaumbwa.


wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana Kondoo aliyechinjwa kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo