Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 6:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Tena usalipo, usiwe kama wanafiki: kwa maana wapenda kusali wakisimama katika sunagogi na katika pembe za njia, illi waonekane na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 “Mnaposali, msifanye kama wanafiki. Wao hupenda kusimama na kusali katika masunagogi na katika pembe za njia ili watu wawaone. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 “Mnaposali, msifanye kama wanafiki. Wao hupenda kusimama na kusali katika masunagogi na katika pembe za njia ili watu wawaone. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 “Mnaposali, msifanye kama wanafiki. Wao hupenda kusimama na kusali katika masunagogi na katika pembe za njia ili watu wawaone. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 “Nanyi mnaposali, msiwe kama wanafiki, maana wao hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Amin nawaambia, wao wamekwisha kupokea thawabu yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 “Nanyi msalipo, msiwe kama wanafiki, maana wao hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Amin nawaambia, wao wamekwisha kupata thawabu yao.

Tazama sura Nakili




Mathayo 6:5
34 Marejeleo ya Msalaba  

Na yo yote mtakayoyaomba katika kusali, mkiamini, mtapokea.


Ole wenu waandisbi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapokea hukumu iliyo kubwa mno.


Tena matendo yao yote huyatenda illi kutazamwa na watu: hupanua fulakteria zao, huongeza matamvna ya mavazi yao;


hupenda mahali pa mbele katika karamu, na viti vya mbele katika sunagogi,


ANGALIENI msitoe sadaka zenu mbele ya watu, kusudi mtazamwe nao: kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.


Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana: maana hujiumbua nyuso zao, illi waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambieni, wamekwisha kupata thawabu yao.


Bassi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika sunagogi na njiani, illi watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao.


Bassi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.


Nanyi, killa msimamapo na kusali, sameheni, kama mkiwa na neno juu ya mtu: illi Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.


Akawaambia katika mafundisho yake, Jibadharini na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni,


Ole wenu, Mafarisayo, kwa sababu mwapenda kukaa mbele katika sunagogi na kusalimiwa masokoni.


AKAWAAMBIA na mfano ya kama imewapasa kumwomba Mungu siku zote wala wasikate tamaa,


Na yule mtoza ushuru akasimama mbali, asitake hatta kuinua macho yake mbinguni; hali akajipigapiga kifua, akisema, Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.


Wanakula nyumba za wajane: na kwa unafiki husali sala ndefu. Hawo watapokea hukumu iliyo kubwa zaidi.


Bali ole wemi ninyi mlio na mali: kwa sababu mmekwisha kuwa na faraja yenu.


Mpaka leo hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, na mtapata, furaha yenu iwe timilifu.


kwa sala zote na kuomha mkisali killa wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo, mkifanya juhudi sana, na kuwaombea watakatifu wote,


Lakini atupa sisi neema nyingi zaidi; kwa hiyo asema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neemi wanyenyekevu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo