Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 5:46 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

46 Maana mkiwapenda wanaowapendani, mwapata thawabu gani? Hatta watoza ushuru, je, nao hawafanyi yayo hayo?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

46 Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda nyinyi? Hakuna! Kwa maana, hata watozaushuru hufanya hivyo!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

46 Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda nyinyi? Hakuna! Kwa maana, hata watozaushuru hufanya hivyo!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

46 Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda nyinyi? Hakuna! Kwa maana, hata watozaushuru hufanya hivyo!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

46 Mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mtapata thawabu gani? Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

46 Kama mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mtapata thawabu gani? Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo?

Tazama sura Nakili




Mathayo 5:46
19 Marejeleo ya Msalaba  

Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakanena, Mlafi huyu, na mnywa mvinyo, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imepewa haki na watoto wake.


Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa: na asipolisikiliza kanisa pia, na awe sawasawa na mtu wa Mataifa na mtoza ushuru.


Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziyada? Hatta wattoza ushuru, je, nao hawafanyi kama hayo?


ANGALIENI msitoe sadaka zenu mbele ya watu, kusudi mtazamwe nao: kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.


Hatta alipokuwa akila nyumbani mwake, watoza ushuru wengi na wenye dhambi waliketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake: kwa maana walikuwa wengi wakamfuata.


Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Kwa nini anakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?


BASSI watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia kumsikiliza.


Na yule mtoza ushuru akasimama mbali, asitake hatta kuinua macho yake mbinguni; hali akajipigapiga kifua, akisema, Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.


Na tazama, mtu mmoja, jina lake alikwitwa Zakkayo, mkubwa wa watoza ushuru, nae tajiri:


Hatta watu walipoona wakanungʼunika wote, wakisema, ya kama, Ameingia akae kwa mtu mwenye dhambi.


Watoza ushuru nao wakaja illi kubatizwa, wakamwambia, Mwalimu, tufanyeni?


Nae Lawi akamfanyia karamu kubwa nyumbani mwake: na palikuwa na kundi kubwa la watoza ushuru, na watu wengine waliokuwa wameketi pamoja nao chakulani.


Mafarisayo na waandishi wao wakawanungʼunikia wanafunzi wake, wakisema, Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?


Watu wote na watoza ushuru waliposikia wakampa Mungu haki, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana.


Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa, mkasema, Mlafi huyu, na mnywaji wa mvinyo, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo