Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 5:29 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

29 Jicho lako la kuume likikukosesha, lingʼoe ulitupe mbali nawe: kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehannum.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Basi, kama jicho lako la kulia linakukosesha, lingoe ukalitupe mbali. Afadhali zaidi kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote kutupwa katika moto wa Jehanamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Basi, kama jicho lako la kulia linakukosesha, lingoe ukalitupe mbali. Afadhali zaidi kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote kutupwa katika moto wa Jehanamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Basi, kama jicho lako la kulia linakukosesha, ling'oe ukalitupe mbali. Afadhali zaidi kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote kutupwa katika moto wa Jehanamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Jicho lako la kuume likikusababisha kutenda dhambi, ling’oe ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima ukatupwa Jehanamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Jicho lako la kuume likikusababisha kutenda dhambi, ling’oe ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima ukatupwa Jehanamu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 5:29
22 Marejeleo ya Msalaba  

Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho: afadhali mmwogopeni yule awezae kuangamiza mwili na roho pia katika jehannum.


Na yu kheri ye yote asiyechukiwa nami.


Kwa maana atafaidiwa mtu nini akiupata ulimwengu wote, na kupata khasara ya roho yake? au mtu atatoa nini badala ya roho yake?


Lakini tusije tukawachukiza, enenda baharini ukatumbukize ndoana, ukatwae samaki yule azukae kwanza; na ukifunua mdomo wake utaona shekeli; ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako.


Maana wako matawashi waliozaliwa katika hali hii toka matumboni mwa mama zao; teua wako matawashi waliofanywa kuwa matawashi na watu: tena wako matawashi waliojifanya kuwa matawashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezae kulipokea neno hili, na alipokee.


Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnazunguka katika bahari na inchi kavu illi kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehannum marra mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.


Enyi nyoka, mazao wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehannum?


Bali mimi nawaambiem, Killa amwoneae ndugu yake ghadhabu bila sababu, itampasa hukumu; na mtu akimwambia ndugu yake, Haka, itampasa baraza; na mtu akinena, Mpumbavu, itampasa jebannum ya moto.


Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe: kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee, wala mwili wako mzima usitupwe katika jehannum.


Maana itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote akapata khasara ya roho yake?


Illa nitawaonya mtakaemwogopa: Mwogopeni yule aliye na uweza baada ya kuua mtu kumtupa katika Jehannum: naam, nawaambieni, Mwogopeni yule.


tukijua haya, ya kuwa mtu wetu wa kale alisulibishwa pamoja nae, illi mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;


kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa: bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.


bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwakhubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.


Nao walio watu wa Kristo Yesu wameusulibisha niwili pamoja na mawazo mabaya na tamaa mbaya.


Bassi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika inchi, uasharati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu:


Tufuate:

Matangazo


Matangazo