Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 5:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Bali mimi nawaambiem, Killa amwoneae ndugu yake ghadhabu bila sababu, itampasa hukumu; na mtu akimwambia ndugu yake, Haka, itampasa baraza; na mtu akinena, Mpumbavu, itampasa jebannum ya moto.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Lakini mimi nawaambieni, yeyote anayemkasirikia ndugu yake, lazima ahukumiwe. Anayemdharau ndugu yake atapelekwa mahakamani. Anayemwita ndugu yake: ‘Pumbavu’ atastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Lakini mimi nawaambieni, yeyote anayemkasirikia ndugu yake, lazima ahukumiwe. Anayemdharau ndugu yake atapelekwa mahakamani. Anayemwita ndugu yake: ‘Pumbavu’ atastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Lakini mimi nawaambieni, yeyote anayemkasirikia ndugu yake, lazima ahukumiwe. Anayemdharau ndugu yake atapelekwa mahakamani. Anayemwita ndugu yake: ‘Pumbavu’ atastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote atakayemkasirikia ndugu yake, atapaswa hukumu. Tena, yeyote atakayemwambia ndugu yake, ‘Raka,’ atapaswa kujibu kwa Baraza la Wayahudi. Lakini yeyote atakayesema ‘Wewe mpumbavu!’ atapaswa hukumu ya moto wa Jehanamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote atakayemkasirikia ndugu yake, atapaswa hukumu. Tena, yeyote atakayemwambia ndugu yake, ‘Raka,’ atapaswa kujibu kwa Baraza la Wayahudi. Lakini yeyote atakayesema ‘Wewe mpumbavu!’ atapaswa hukumu ya moto wa Jehanamu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 5:22
93 Marejeleo ya Msalaba  

Jihadharini na wana Adamu; kwa maana watawapelekeni mbele ya baraza, na katika masunagogi yao watawapiga;


Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho: afadhali mmwogopeni yule awezae kuangamiza mwili na roho pia katika jehannum.


Lakini Mafarisayo waliposikia, wakasema, Huyu hafukuzi pepo, illa kwa uweza wa Beelzebul mkuu wa pepo.


Alipokuwa akisema, wingu jeupe likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, niliyependezwa nae; msikieni yeye.


Kiisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu akinitenda dhambi nimsamehe marra ngapi? hatta marra saba?


Vivyo hivyo na Baba yangu wa mbinguni atawatenda ninyi, kama ninyi kwa mioyo yenu hamkusamehe killa mtu ndugu yake makosa yake.


Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnazunguka katika bahari na inchi kavu illi kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehannum marra mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.


Enyi nyoka, mazao wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehannum?


Kisha atawaambia na wale walio mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, kwenda katika moto wa milele, aliowekewa tayari Shetani na malaika zake:


Makuhani wakuu na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa nwongo juu ya Yesu, wapate kumwua;


na sauti toka mbinguni ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninaependezwa nae.


bali mimi nawaambieni, Usiape kabisa; hatta kwa mbingu, kwa maana ndio kiti cha enzi cha Mungu;


bali mimi nawaambieni, Wapendeni adui zenu, wabarikini wanaowalaani, watendeni mema wanaowachukia, waombeeni wanaowatendea ukorofi, na kuwatesa;


Makuhani wakuu na baraza wote wakatafuta ushuhuda juu ya Yesu wapate kumwua: wasione.


MARRA ilipokuwa assubuhi makuhani wakuu wakafanya shauri pamoja na wazee na waandishi na haraza zima, wakamfunga Yesu, wakamchukua, wakamleta kwa Pilato.


Illa nitawaonya mtakaemwogopa: Mwogopeni yule aliye na uweza baada ya kuua mtu kumtupa katika Jehannum: naam, nawaambieni, Mwogopeni yule.


Hatta ulipokuwa mchana wakakusanyika jamii ya wazee wa watu, na makuhani wakuu, na waandishi, wakamleta kwa haraza yao, wakisema,


Bassi makuhani wakuu na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakanena, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi.


Lakini litimie neno lililoandikwa katika sharia yao, Walinichukia burre.


Makutano wakajibu, wakasema, Una pepo; ni nani anaetafuta kukuua?


Wayahudi wakajibu wakamwambia, Hatuneni vema sisi kwamba wewe u Msamaria, na una pepo?


Na baadhi ya Waepikurio na Wastoiko, matilosofo, wakakutana nae. Wengine wakasema, Mtu huyu mwenye maneno mengi anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza khabari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akikhubiri khabari za Yesu na ufufuo.


Siku ya pili yake akitaka kujua hakika, ni kwa sababu gani ameshitakiwa na Wayahudi, akamfungua, akawaamuru makuhani wakuu na baraza yote waje. Akamleta Paolo chini, akamweka mbele yao.


PAOLO akawakazia macho watu wa baraza, akasema, Ndugu zangu, mimi kwa nia safi kabisa nimeishi mbele za Mungu hatta leo hivi.


Au watu hawa wenyewe na waseme, ni kosa gani waliloliona kwangu niliposimama mbele ya baraza,


Wakawaamuru kutoka katika baraza, wakafanya shauri, wakisemii, Tuwafanyieni watu hawa?


Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja kuhani mkuu nao walio pamoja nae, wakawaita watu wa haraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani illi wawalete.


Wakawaleta, wakaweka katika baraza. Kuhani mkuu akawauliza, akisema,


Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi: wakaniwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza.


Watu wote walioketi katika ile baraza wakamkazia macho yao, wakamwona uso wake kuwa kama uso wa malaika.


Musa huyo ndiye aliyewaambia wana wa Israeli, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii katika ndugu zenu, kama mimi: mtamsikia huyo.


Kwa pendo la udugu, mwe na shauku ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;


wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyangʼanyi.


Bali mwashitakiana, ndugu na ndugu, tena mbele yao wasioamini.


mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizae kisasi cha haya yote, kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudu sana.


wasimtukane mtu, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.


Angalieni msimkatae yeye anenae. Maana ikiwa wale hawakuokoka waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya inchi, sembuse sisi tukijiepusha nae atuonyae kutoka mbinguni:


nae alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokofu wa milele kwa watu wote wanaomtii;


Lakini wataka kujua, wewe mwana Adamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?


Kaangalieni jinsi moto mdogo uwasbavyo kuni nyingi sana. Nao ulimi ni moto, ulimwengu wa uovu. Ndio khabari ya ulimi katika viungo vyetu, huutia najis mwili wote, huliwasha moto gurudumu la maumbile, nao huwashwa moto na jehannum.


yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki;


watu wasiolipa baya badala ya baya, au laumu badala ya laumu; bali wabarikio; kwa sababu ndiyo mlioitiwa illi mrithi baraka.


Yeye asemae kwamba yumo katika nuru, nae amchukia ndugu yake, yumo gizani hatta sasa.


Hivi watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Shetani. Mtu aliye yote asiyefanya haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.


Mtu akimwona ndugu yake anakosa kosa lisilo la mauti, ataomba, nae atampa uzima kwa ajili ya hawo wakosao kosa lisilo la mauti. Liko kosa lililo la mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hilo.


Lakini Mikael, malaika mkuu, aliposhindana na Shetani, na kuhujiana nae kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana akukemee.


Mauti na Kuzimu wakatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo