Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 5:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 Maana nawaambieni, Haki yenu isipozidi kuliko haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Ndio maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa waalimu wa sheria na wa Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Ndio maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa waalimu wa sheria na wa Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Ndio maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa waalimu wa sheria na wa Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Kwa maana nawaambia, haki yenu isipozidi haki ya Mafarisayo na walimu wa Torati, kamwe hamtaingia katika ufalme wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Kwa maana nawaambia, haki yenu isipozidi haki ya Mafarisayo na walimu wa Torati, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni.

Tazama sura Nakili




Mathayo 5:20
24 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo wakafahamu ya kuwa hakuwaambia kujihadhari na chachu ya mkate, bali elimu ya Mafarisayo na Masadukayo.


Na ye yote atakaepokea kitoto kimoja mfano wa hiki kwa jina langu, anipokea mimi:


Nalo shoka limekwisha kuwekwa penye shina la miti; bassi killa mti usiozaa matunda mazuri unakatwa na kutupwa motoni.


Siye killa mtu aniambiae, Bwana, Bwana, atakaeingia katika ufalme wa mbinguni; hali yeye afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.


Amin, nawaambieni, Yeye yote asiyeukubali nfalme wa Mungu kama mtoto mchanga hatauingia kabisa.


Ni rakhisi ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.


Ole wenu, maana mfano wenu ni makaburi yasiyoonekana, na watu wapitao juu yao hawana khabari.


HUKO nyuma mkutano wa watu, watu elfu nyingi walipokusanyika hatta wakakanyagana, akaanza kuwaambia wanafunzi wake khassa, Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki.


Amin, nawaambieni, Yeye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto, hatauingia kamwe.


Kwa maana ikiwa khuduma ya hukumu ina utukufu, khuduma ya haki ina utukufu unaozidi sana.


Hatta imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo ni kiumbe kipya, vya kale vimepita; kumbe! vyote vimekuwa vipya.


tena nionekane katika yeye, nisiwe na baki ile ipatikanayo kwa sharia, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani;


Fanyeni bidii kutafuta amani kwa watu wote, na utakatifu, ambao hapana mtu atakaemwona Mungu asipokuwa nao;


Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyae machukizo na uwongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo