Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 5:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Bassi mtu atakaevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha wafu hivi, atakwitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni: bali mtu atakaezitenda na kufundisha, huyu afakwitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine, huyo atakuwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine, huyo atakuwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine, huyo atakuwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Kwa hiyo, yeyote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni, lakini yeyote azitendaye na kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu katika ufalme wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Kwa hiyo, yeyote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni, lakini yeyote azitendaye na kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu katika Ufalme wa Mbinguni.

Tazama sura Nakili




Mathayo 5:19
38 Marejeleo ya Msalaba  

Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji: illakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.


Yesu akamwambia, Amin, nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata, katika zamani za kuzaliwa upya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli.


Lakini kwemi ninyi haitakuwa hivi: bali ye yote atakae kuwa mkuu kwenu, na awe mkhudumu wenu;


mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi: nti tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hatta mwisho wa dunia. Amin.


Kwa maani atakuwa mkuu mbele ya Mungu, hatakunywa divai wala kileo: nae atajazwa Roho Mtakatifu hatta tangu tumbo la mama yake.


Bali ole wenu Mafarisayo, kwa sababu mnalipa zaka za mnaana na mchicha, na killa mboga, mkaacha adili na upendo wa Mungu: iliwapaseni kuyafanya haya ya kwanza bila kuacha haya ya pili.


akawaambia, Killa mtu atakaempokea kitoto hiki kwa jina langu, anipokea mimi, na killa mtu atakaenipokea mimi, ampokea yeye aliyenituma. Maana yeye aliye mdogo miongoni mwenu ninyi nyote, huyu atakuwa mkubwa.


KITABU kile cha kwanza nalikifanya, Theofilo, katika khabari ya mambo yote aliyoanza kufanya Yesu na kufundisha,


Kwa maana tusiseme (kama tulivyosingiziwa nakama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba sisi twanena), Na tufanye mabaya, illa yaje mema? kuhukumiwa kwao kuna haki.


TUSEME nini bass? Tudumu katika dhambi illi neema iwe nyingi zaidi?


Ni nini bassi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sharia bali chini ya neema? Hasha!


Bali wewe, mtu wa Mungu, yakimbie hayo, ukafuate haki, utawa, imani, upendo, uvumilivu, upole.


Neno hili ni amini, na mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu, illi wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Haya ni mazuri, tena yana faida kwa wana Adamu.


Na mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka.


Killa afanyae dhambi, afanya nasi; kwa kuwa dhambi ni nasi.


Lakini nina maneno machache juu yako, ya kwamba wamwacha yule mwanamke Yezebel, yeye ajiitae nabii, nae awafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, illi wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo