Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 4:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Khabari zake zikaenea katika Sham yote; wakamletea watu waliokuwa hawawezi, walioshikwa mi maradhi mbali mbali na mateso, nao wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Habari zake zikaenea pande zote za Siria. Wagonjwa wote wenye maradhi ya kila namna na wale waliosumbuliwa na kila namna ya taabu: Waliopagawa na pepo, wenye kifafa na watu waliokuwa wamelemaa, walipelekwa kwake; naye akawaponya wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Habari zake zikaenea pande zote za Siria. Wagonjwa wote wenye maradhi ya kila namna na wale waliosumbuliwa na kila namna ya taabu: Waliopagawa na pepo, wenye kifafa na watu waliokuwa wamelemaa, walipelekwa kwake; naye akawaponya wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Habari zake zikaenea pande zote za Siria. Wagonjwa wote wenye maradhi ya kila namna na wale waliosumbuliwa na kila namna ya taabu: waliopagawa na pepo, wenye kifafa na watu waliokuwa wamelemaa, walipelekwa kwake; naye akawaponya wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Kwa hiyo sifa zake zikaenea sehemu zote za Siria, nao watu wakamletea wote waliokuwa na magonjwa mbalimbali na maumivu, waliopagawa na pepo wachafu, wenye kifafa na waliopooza, naye akawaponya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Kwa hiyo sifa zake zikaenea sehemu zote za Shamu, nao watu wakamletea wote waliokuwa na magonjwa mbalimbali na maumivu, waliopagawa na pepo wachafu, wenye kifafa na waliopooza, naye akawaponya.

Tazama sura Nakili




Mathayo 4:24
41 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu na bubu; akamponya, hatta yule kipofu na bubu akasema na kuona.


WAKATI ule Herode tetrarka alisikia khabari za Yesu,


Na mwanamke Mkauanaya wa mipaka ile akatokea, akampaazia sauti, akinena, Unirehemu. Bwana, Mwana wa Daud; binti yangu amepagawa sana na pepo.


Bwana, mrehemu mwana wangu, kwa kuwa hushikwa na kifafa, na kuteswa vibaya: maana marra nyingi huanguka motoni, na marra nyingi majini.


Yesu akamkaripia pepo, akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile.


Yesu akazunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika sunagogi zao, na kuikhubiri injili ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa killi namna katika watu.


Alipofika ngʼambu, katika inchi ya Wagergesene, watu wawili wenye pepo walikutana nae, wanatoka makaburini, wakali mno, hatta mtu asiweze kupita njia ile.


Wachungaji wakakimbia, wakaenda zao mjini, wakayakhubiri yote, na mambo ya wenye pepo pia.


akinena, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.


Zikaenea khabari hizi katika inchi ile yote.


Na Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masunagogi yao, akikhubiri injili ya ufalme, akiponya magonjwa yote na dhaifu zote katika watu.


Khahari zake zikaenea marra inchi zote kando ya Galilaya.


Hatta ilipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, wakamletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo.


Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wane.


Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu va makutano, wakaitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakakitelemsha kitanda alichokilalia yule mwenye kupooza.


Vipi vyepesi, kumwambia mwenye kupooza, Dhambi zako zimeondolewa, au kusema, Ondoka, njitwike kitanda chako, ukaenende?


orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa wakati Kurenio alipotawala Sham.


Yesu akarudi kwa nguvu za Roho hatta Galilaya, khabari zake zikaenea katika inchi yote iliyo kando kando.


Akatoka katika sunagogi, akaingia nyumba ya Simon. Bassi mkwewe Simon alikuwa ameshikwa na homa kali, wakamwomba kwa ajili yake.


Lakini khabari zake zikazidi kuenea, wakakutana makutano mengi kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.


Lakini mpate kujua ya kuwa Mwana wa Adamu ana mamlaka duniani ya kuondoa dhambi (alimwambia yule mwenye kupooza), Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako ukaende nyumbani kwako.


Zikatoka hizo khabari zake katika Yahudi yote, na katika inchi yote iliyozunguka.


Wengine wakasema, Maneno haya siyo ya mtu mwenye pepo. Je! pepo aweza kuwafumbua macho vipofu?


khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae.


Wakaandika hivi kwa mikono yao, Mitume na wazee na ndugu, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shami na Kilikia, walio wa mataifa, salamu.


Akapita katika Shami na Kilikia akawatia moyo makanisa.


Yalipokwisha kutendeka hayo wengine waliokuwa na magonjwa katika kisiwa wakaja wakaponywa; nao wakatuheshimu kwa heshima nyingi.


Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu: na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo