Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 4:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Yesu akazunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika sunagogi zao, na kuikhubiri injili ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa killi namna katika watu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Yesu alikuwa anakwenda kila mahali wilayani Galilaya, akifundisha katika masunagogi na kuhubiri Habari Njema juu ya ufalme wa Mungu. Aliponya kila namna ya maradhi na magonjwa waliyokuwa nayo watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Yesu alikuwa anakwenda kila mahali wilayani Galilaya, akifundisha katika masunagogi na kuhubiri Habari Njema juu ya ufalme wa Mungu. Aliponya kila namna ya maradhi na magonjwa waliyokuwa nayo watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Yesu alikuwa anakwenda kila mahali wilayani Galilaya, akifundisha katika masunagogi na kuhubiri Habari Njema juu ya ufalme wa Mungu. Aliponya kila namna ya maradhi na magonjwa waliyokuwa nayo watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Isa akazunguka Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri Habari Njema za ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi miongoni mwa watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Isa akapita katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema za Ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi miongoni mwa watu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 4:23
46 Marejeleo ya Msalaba  

vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanakhubiriwa khabari njema.


Akaondoka huko, akaiugia katika sunagogi lao.


Killa alisikiae neno la ufalme asifahamu, huja yule mwovu, akaliteka lililopandwa moyoni mwake. Huyu ndiye aliyepandwa njiani.


Na alipofika inchi yake, akawafundisha katika sunagogi yao, hatta wakashangaa, wakanena, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii?


Yesu akatoka, akaona makutano mengi, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao.


Na injili hii ya ufalme itakhubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; ndipo ule mwisho utakapokuja.


Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


Na Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masunagogi yao, akikhubiri injili ya ufalme, akiponya magonjwa yote na dhaifu zote katika watu.


Hatta baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiikhubiri injili ya ufalme wa Mungu,


Wakashika njia hatta Kapernaum; na siku ya sabato akaingia sunagogi, akafundisha.


Akawa akikhubiri katika masuuagogi yao, katika inchi yote ya Galilaya, na kufukuza pepo.


Maana aliponya wengi, hatta wote waliokuwa na misiba wakamrukia wapate kumgusa.


Ilipokuwa sabato, akaanza kufundisha katika sunagogi: wengi wakisikia, wakashangaa, akinena, Huyu amepata wapi haya? Na, Hekima gani hii aliyopewa huyu, na nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?


Akastaajahu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Akazungukazunguka katika vile vijiji, akifundisha.


Waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni ya kama, Ufalme wa Mungu umewakaribieni.


Akawa akifundisha katika sunagogi mojawapo siku ya sabato.


Torati na manabii zilikuwako mpaka Yohana. Tangu wakati ule, khabari njema ya ufalme wa Mungu inakhubiriwa, na killa mtu anauingia kwa nguvu.


IKAWA siku moja, alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni na kuikhubiri Injili, makuhani wakuu na waandishi, na pamoja nao wazee, wakamtokea ghafula,


Yesu akarudi kwa nguvu za Roho hatta Galilaya, khabari zake zikaenea katika inchi yote iliyo kando kando.


Hatta siku moja ya siku zile alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waandishi wameketi, waliokuwa wametoka katika killa kijiji cha Galilaya, na cha Yahudi, na Yerusalemi; uweza wa Bwana ulikuwa pamoja nae apate kuwaponya.


Akatelemka pamoja nao, akasimama panapo uwanda, pamoja na kundi la wanafunzi wake, na kundi la watu waliotoka Yahudi wote, na Yerusalemi, na pwani ya Turo na Sidon, waliokuja wamsikilize na kuponywa maradhi zao;


Ikawa Sabato nyingine akaingia katika sunagogi, akafundislia: na palikuwako huko mtu mwenye mkono umepooza, mkono wa kuume.


Saa ileile akawaponya watu wengi maradhi zao, na misiba yao, na pepo wabaya: na vipofu wengi akawakarimia kuona.


Akajibu, akawaambia, Enendeni, mkamweleze Yohana mliyoyaona na kuyasikia: vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanakhubiriwa khahari njema:


IKAWA muda si muda alikuwa akizungukazunguka katika miji na vijiji, akikhutubu na kukhubiri khabari njema za ufalme wa Mungu. Na wale thenashara walikuwa pamoja nae,


Namakutano walipojua wakamfuata: akawakaribisha, akanena nao khabari za ufalme wa Mungu, akawaponya waliokuwa na haja ya kuponywa.


Akamwambia, Waache wafu wazike wafu wao, bali wewe enenda zako ukautangaze ufalme wa Mungu.


Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu kwa wazi; mimi siku zote nalifundisha katika masunagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi siku zote; wala kwa siri sikusema neno.


Maneno haya aliyasema sunagogini, alipokuwa akifundisha huko Kapenaum.


NA baada ya haya Yesu akawa akitembea katika Galilaya: maana hakutaka kutembea katika Yahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua.


khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae.


Akatoa hoja zake katika sunagogi killa sabato akawavuta Wayahudi na Wayunani waamini.


Na sasa mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowakhubirini ufalme wa Mungu, nikienda huko na huko, hamtaniona uso tena.


Tena wakhubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri namna gani miguu yao wakhubirio khabari ya mema.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo