Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 3:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 msiwaze moyoni kwamba, Tuna baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambieni ya kwamba Mungu anaweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Msifikiri na kujisemea, ‘Baba yetu ni Abrahamu!’ Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Msifikiri na kujisemea, ‘Baba yetu ni Abrahamu!’ Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Msifikiri na kujisemea, ‘Baba yetu ni Abrahamu!’ Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Wala msidhani mnaweza kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Ibrahimu, baba yetu.’ Nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto kutoka kwa mawe haya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Wala msidhani mnaweza kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Ibrahimu, baba yetu.’ Nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto kutoka kwa mawe haya.

Tazama sura Nakili




Mathayo 3:9
22 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, zina, asharati,


Akaanza kuwaza moyoni, akisema, Nifanyeje, maana sina pa kuweka akiba mavuno yangu?


Akalia, akasema, Baba Ibrahimu, unirehemu, umtume Lazaro, achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa maana naumia katika moto huu.


Akajibu, akasema, Nawaambieni kwamba, wakinyamaza hawa, mawe yatapiga kelele.


Zaeni, bassi, matunda yapatanayo na toba wala msianze kusema ndani ya nafsi zenu, Tunae baba ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambieni, ya kwamba Mungu katika mawe haya aweza kumwinulia Ibrahimu watoto.


Yesu akafahamu fikara zao akajibu, akawaambia, Mnafikiri nini mioyoni mwenu?


Yule Farisayo aliyemwalika, alipoona haya akasema kimoyomoyo, akinena, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angalimjua huyu ni nani! na ni mwanamke gani anaemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi.


Wakamjihu, Tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wanenaje, Mtawekwa huru?


Najua ya kuwa m mzao wa Ibrahimu; lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halina nafasi ndani yenu.


Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, nae amekufa? Na manabii wamekufa; wajifanya kuwa nani?


Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, nao miongoni mwenu mnaomcha Mungu, kwenu ninyi neno la wokofu huu limepelekwa.


Simeon ametueleza jinsi Mungu alivyowaangalia mataifa illi achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake.


BASSI, tusemeje? Ibrahimu baba yetu kwa jinsi ya mwili amepata nini?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo