Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 3:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Hatta akiona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, akawaambia, Uzao wa nyoka, nani aliyewaonya mkimbie ghadhabu ijayo?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo wanamjia ili awabatize, aliwaambia, “Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea muikimbie ghadhabu inayokuja?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo wanamjia ili awabatize, aliwaambia, “Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea muikimbie ghadhabu inayokuja?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo wanamjia ili awabatize, aliwaambia, “Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea muikimbie ghadhabu inayokuja?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Lakini alipowaona Mafarisayo na Masadukayo wengi wakija ili kubatizwa, aliwaambia: “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Lakini alipowaona Mafarisayo na Masadukayo wengi wakija ili kubatizwa, aliwaambia: “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja?

Tazama sura Nakili




Mathayo 3:7
49 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Mafarisayo waliposikia, wakasema, Huyu hafukuzi pepo, illa kwa uweza wa Beelzebul mkuu wa pepo.


Uzao wa nyoka, mwawezaje kusema mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.


Ndipo wanafunzi wake wakamwendea, wakamwambia, Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile walichukizwa?


WAKAMJIA Mafarisayo na Masadukayo, wakamjaribu, wakamwomba awaonyeshe ishara itokayo mbinguni.


Yesu akawaambia, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masudukayo.


Ndipo Mafarisayo wakaenda zao, wakafauya shauri, jinsi ya kumtega kwa maneno.


Siku ile Masadukayo, watu wanenao kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza,


Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, wakakusanyika pamoja.


Enyi nyoka, mazao wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehannum?


Maana nawaambieni, Haki yenu isipozidi kuliko haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.


Wakatuma kwake baadhi ya Mafarisayo na Maherodiano, illi wamnase kwa maneno.


Na Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hapana kiyama, wakamwendea,


Akawaagiza, akisema, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode.


Mafarisayo nao wakayasikia haya yote, nao walikuwa wakipenda fedha; wakamdhihaki.


Yule Farisayo akasimama, akasali hivi kwa nafsi yake, Mungu, nakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine, wanyangʼanyi, wazinzi, waia kama na huyu mtoza ushuru.


Bali Mafarisayo na wana sharia walijikatalia shauri la Mungu kwa kuwa hawakubatizwa nae.


Nao waliotumwa walitoka kwa Mafarisayo.


Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo.


Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pamoja nae wakasikia haya, wakamwambia, Je! sisi nasi tu vipofu?


Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika Torati ya Musa.


Kwa biyo kesheni, mkikumbuka kama miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya killa mtu kwa machozi.


wakinijua sana tangu mwanzo, kama wakipenda kushuhudia, ya kwamba nalikuwa Farisayo kwa kuifuata madhehebu ya dini yetu iliyo sahihi kabisa.


Akaondoka kuhani mkuu na wote waliokuwa pamoja nae (hao ndio walio wa madhehehu ya Masadukayo) wamejaa wivu,


Kwa maana ghadhahu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wana Adamu waipingao kweli kwa uovu wao.


Bassi zaidi sana tukiisha kupewa haki katika damu yake tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.


na kumugojea Mwana wake kutoka mbinguni, ambae alimfufua katika wafu, Yesu, anaetuokoa na ghadhabu itakayokuja.


Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu khabari za mambo yasiyoonekana bado, kwa kumcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Kwa hiyo akauhukumu ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.


illi kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu bawezi kusema nwongo, tupate faraja lililo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;


Hivi watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Shetani. Mtu aliye yote asiyefanya haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo