Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 3:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Mimi ninawabatizeni kwa maji kuonesha mmetubu. Lakini anayekuja baada yangu ana nguvu kuliko mimi, nami sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Mimi ninawabatizeni kwa maji kuonesha mmetubu. Lakini anayekuja baada yangu ana nguvu kuliko mimi, nami sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Mimi ninawabatizeni kwa maji kuonesha mmetubu. Lakini anayekuja baada yangu ana nguvu kuliko mimi, nami sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 “Mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini nyuma yangu anakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuvichukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu wa Mungu na kwa moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 “Mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini nyuma yangu anakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuvichukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho wa Mwenyezi Mungu na kwa moto.

Tazama sura Nakili




Mathayo 3:11
29 Marejeleo ya Msalaba  

wakabatizwa nae mtoni Yordani, wakiziungama dhambi zao.


Akatokea Yohana, akibatiza jangwani, na kuukhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi.


Nae atatangulia mbele ya uso wake, mwenye roho ya Eliya, na nguvu zake, kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na kuwageuza maasi waelekee akili zao wenye haki; illi kumfanyia tayari Bwana watu waliotengenezwa.


Yohana akajibu, akawaambia wote, Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yuaja aliye hodari kuliko mimi, ambae kwamba mimi sistahili kumfungulia ukanda wa viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto:


Akalika inchi yote iliyo kando ya Yardani, akikhuhiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi,


Yohana akamshuhudia, akapaaza sauti yake, akinena, Huyu ndiye niliyemnena khabari zake, kwamba, Ajae nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.


Huyu ndiye niliyemnena khabari zake, Yuaja mtu nyuma yangu, aliyekuwa mbele yangu, kwa maana alikuwa kabla yangu.


ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi si nyingi.


Paolo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakaekuja nyuma yake, yaani Kristo Yesu.


Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji: yule tawashi akasema, Yanizuia nini nisibatizwe?


Akaamuru lile gari lisimame: wakatelemka wote wawili majini. Filipo na yule tawashi: akambatiza.


Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa tukaingia katika mwili mmoja, ikiwa tu Wayahudi, au ikiwa tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.


Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii, kuwakhubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;


alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda, bali kwa rehema yake, kwa josho la kuzaliwa kwa pili, na kufanywa upya na Roho Mtakatifu,


Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu kama mshipi, mpate kukhudumiana; kwa sababu Mungu hushindana na wenye kiburi, huwapa wanyenyekevu neema.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo