Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 28:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Nao walipokuwa wakienda kuwapasha wanafunzi wake khabari, Yesu akakutana nao, akinena, Salam! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Mara, Yesu akakutana nao, akasema: “Salamu.” Hao wanawake wakamwendea, wakapiga magoti mbele yake, wakashika miguu yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Mara, Yesu akakutana nao, akasema: “Salamu.” Hao wanawake wakamwendea, wakapiga magoti mbele yake, wakashika miguu yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Mara, Yesu akakutana nao, akasema: “Salamu.” Hao wanawake wakamwendea, wakapiga magoti mbele yake, wakashika miguu yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Ghafula, Isa akakutana nao, akasema, “Salamu!” Wale wanawake wakamkaribia, wakaishika miguu yake, wakamwabudu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Ghafula, Isa akakutana nao, akasema, “Salamu!” Wale wanawake wakamkaribia, wakaishika miguu yake, wakamwabudu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 28:9
18 Marejeleo ya Msalaba  

Nao waliokuwa ndani ya chombo wakamwendea, wakamsujudia, wakinena, Hakika wewe u Mwana wa Mungu.


na kusalimiwa sokoni, na kuitwa na watu, Rabbi, Rabbi.


Yesu akawaambia, Msiogope: enendeni, mkawaambie ndugu zangu waemle Galilaya, ndiko watakakoniona.


Nao walipomwona, wakamsujudia; lakini wengine waliona shaka.


Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa khofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake khabari.


Akaja kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe.


Nao wakamsujudia, wakarudi Yerusalemi na furaha kuu:


akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumchuruzia miguu kwa machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake akibusu sana miguu yake, na kuipaka yale marhamu.


Bassi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akaifuta miguu yake kwa nywele zake; nyumha ikajaa harufu ya yale marhamu.


Ikawa jioni katika siku ile ya kwanza ya sabato, na milango imefungwa walipokuwapo wanafunzi kwa khofu ya Wayahudi, akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani kwenu.


Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu, na Mungu wangu.


Khatimae, ndugu, kwa kherini; mtimilike, mfarajike, nieni mamoja, mkae katika imani; na Mungu wa upendo na amani awe pamoja nanyi.


Tazama, nakupa walio wa sunagogi la Shetani, wasemao kwamba wao ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uwongo. Tazama, nitawafanya waje wasujudu mbele ya miguu yako na kujua ya kuwa nimekupeuda.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo