Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 28:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Hayupo hapa; kwa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni, patazameni mahali alipolazwa Bwana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Hayupo hapa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni mkaone mahali alipokuwa amelala.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Hayupo hapa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni mkaone mahali alipokuwa amelala.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Hayupo hapa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni mkaone mahali alipokuwa amelala.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Hayupo hapa, kwa kuwa amefufuka, kama alivyosema. Njooni mpatazame mahali alipokuwa amelazwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Hayupo hapa, kwa kuwa amefufuka, kama vile alivyosema. Njooni mpatazame mahali alipokuwa amelazwa.

Tazama sura Nakili




Mathayo 28:6
17 Marejeleo ya Msalaba  

Maana kama vile Yunus alivyokuwa siku tatu mchana na nsiku katika tumbo la nyamgumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa inchi.


Toka wakati huo Yesu akaanza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemi, na kuteswa mengi na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.


nao watamwua, na siku ya tatu atafufuka. Wakasikitika sana.


Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu akawaagiza, akinena, Msimwambie mtu khabari ya mambo hayo, hatta Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.


na watampeleka kwa Mataifa wapate kumdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumsulibi; na siku ya tatu atafufuka.


wakinena, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa hayi bado, Baada ya siku tatu nitafufuka.


Nae akawaambia, Msistaajabu; muamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa: amefufuka: bayupo hapa: patazameni pahali walipomweka.


Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na makuhani, wakuu na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka.


Lakini Petro akaondoka, akaenda mbio kaburini, akainama, akachungulia ndani, akaviona vile vitambaa vimewekwa peke yake, akarudi kwake, akistaajabu kwa yale yaliyotokea.


wasioukuta mwili wake, wakaja, wakasema ya kwamba wametokewa na malaika, waliowaambia yu hayi.


Akawaambia, Haya ndiyo maneno yangu niliyowaambieni, nilipokuwa kwenu, ya kuwa hayana buddi kutimizwa yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii, na katika zaburi.


Ndio maana Baba anipenda, kwa sababu nauweka uzima wangu illi niutwae tena.


Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hii, nami kwa siku tatu nitaisimamisha.


Mungu akamfufua, akilegeza utungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo