Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 27:54 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

54 Bassi yule akida, nao walio pamoja nae wakimwangalia Yesu, walipoliona tetemeko la inchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakinena, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

54 Basi, jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesu walipoona tetemeko la ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

54 Basi, jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesu walipoona tetemeko la ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

54 Basi, jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesu walipoona tetemeko la ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

54 Basi yule jemadari na wale waliokuwa pamoja naye wakimlinda Isa walipoona lile tetemeko na yale yote yaliyokuwa yametukia, waliogopa sana, wakapaza sauti na kusema, “Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

54 Basi yule jemadari na wale waliokuwa pamoja naye wakimlinda Isa walipoona lile tetemeko na yale yote yaliyokuwa yametukia, waliogopa, wakasema, “Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”

Tazama sura Nakili




Mathayo 27:54
22 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Yesu akanyamaza. Kuhani mkuu akamjihu, akamwambia, Nakuapisha Mungu aliye hayi, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.


Wakaketi, wakamwangalia huko.


wakinena, Ewe ulivunjae hekalu na kuijenga kwa siku tatu, jiponye nafsi yako; ukiwa Mwana wa Mungu, shuka msalahani.


Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kamii akimtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu.


Na tazama pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hatta chini: inchi ikatetema; miamba ikapasuka;


Mjaribu akamjia akasema, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.


Hatta Yesu alipoingia Kapernaum, akida alimjia, akamsihi,


Bassi yule akida, aliyesimama akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa, Mwana wa Mungu.


Wakasema wote, Bassi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mnasema kama mimi ndiye.


Wayahudi wakamjibu, Sisi tuna sharia, na kwa sharia hiyo amepasiwa kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu.


PALIKUWA na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitaliano,


Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?


Marra hiyo akatwaa askari na maakida, akawashukia mbio. Nao walipomwona jemadari na askari wakaacha kumpiga Paolo.


Paolo akamwita akida mmoja, akasema, Mchukue huyu kwa jemadari; maana ana neno la kumwarifu.


Akaita maakida wawili, akasema, Wekeni tayari askari miateen kwenda Kaisaria, na askari wapanda farasi sabaini, na wenye mikuki miateen, panapo saa tatu ya usiku.


BASSI ilipoamriwa tusafiri hatta Italia, wakamtia Paolo na wafungwa wengine katika mikono ya akida mmoja, jina lake Yulio, wa kikosi cha Augusto.


Bali akida, akitaka kumponya Paolo, akawazuia, wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea wajitupe baharini, wafike inchi kavu;


na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo; Yesu Kristo Bwana wetu,


Na katika saa ile palikuwa na tetemeko la inchi, nalo kubwa, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka, wana Adamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na khofu wakamtukuza Mungu wa mbingu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo