Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 27:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Ndipo Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu na wazee vile vipande thelathini vya fedha,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Hapo, Yuda, ambaye ndiye aliyemsaliti, alipoona kwamba wamekwisha mhukumu Yesu, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu vile vipande thelathini vya fedha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Hapo, Yuda, ambaye ndiye aliyemsaliti, alipoona kwamba wamekwisha mhukumu Yesu, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu vile vipande thelathini vya fedha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Hapo, Yuda, ambaye ndiye aliyemsaliti, alipoona kwamba wamekwisha mhukumu Yesu, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu vile vipande thelathini vya fedha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Yuda, aliyemsaliti Isa, alipoona kuwa Isa amehukumiwa, akajuta na akarudisha vile vipande thelathini vya fedha alivyopewa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Yuda, ambaye alikuwa amemsaliti Isa, alipoona kuwa Isa amehukumiwa, akajuta na akarudisha vile vipande thelathini vya fedha alivyopewa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 27:3
15 Marejeleo ya Msalaba  

Hatta wakati wa chakula cha jioni, Shetani alipokwisha kumtia Yuda, mwana wa Simon Iskariote, moyo wa kumsaliti,


Na baada ya lile tonge, Shetani akamwingia. Bassi Yesu akamwambia, Uyatendayo, yatende upesi.


Bassi Yuda akiisha kupokea kikosi cha askari, na watumishi waliotoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo, akaenda huko na makandili na taa za mkono na silaha.


(Bassi huyu alinunua konde kwa ijara ya ndhalimu; akaanguka kifudifudi akapasuka, matumbo yake yote yakatoka.


Maana huzuni iliyo mbele za Mungu hufanyiza toba iletayo wokofu isiyo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanyiza mauti.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo