Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 27:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Pilato alipoona ya kuwa hafai neno, bali ya kuwa inazidi kuwa ghasia, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya makutano, akasema, Mimi sina khatiya kwa khabari ya damu ya mtu huyu mwenye haki: tazameni hayo ninyi wenyewe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Basi, Pilato alipotambua kwamba hafanikiwi chochote na kwamba maasi yalikuwa yanaanza, alichukua maji, akanawa mikono mbele ya ule umati wa watu, akasema, “Mimi sina lawama juu ya kifo cha mtu huyu; shauri lenu wenyewe.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Basi, Pilato alipotambua kwamba hafanikiwi chochote na kwamba maasi yalikuwa yanaanza, alichukua maji, akanawa mikono mbele ya ule umati wa watu, akasema, “Mimi sina lawama juu ya kifo cha mtu huyu; shauri lenu wenyewe.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Basi, Pilato alipotambua kwamba hafanikiwi chochote na kwamba maasi yalikuwa yanaanza, alichukua maji, akanawa mikono mbele ya ule umati wa watu, akasema, “Mimi sina lawama juu ya kifo cha mtu huyu; shauri lenu wenyewe.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Pilato alipoona kwamba hawezi kufanya lolote, lakini badala yake ghasia zilikuwa zinaanza, akachukua maji, akanawa mikono yake mbele ya umati wa watu, akasema, “Sina hatia kwa damu ya mtu huyu, hili ni jukumu lenu!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Pilato alipoona kwamba hawezi kufanya lolote, lakini badala yake ghasia zilikuwa zinaanza, akachukua maji, akanawa mikono yake mbele ya ule umati wa watu, akasema, “Sina hatia juu ya damu ya mtu huyu, hili ni jukumu lenu!”

Tazama sura Nakili




Mathayo 27:24
16 Marejeleo ya Msalaba  

Wakanena, Sio wakati wa siku kuu, isije ikatokea ghasia katika watu.


Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki: kwa sababu nimeteswa mengi leo katika udoto kwa ajili yake.


Liwali akasema, Kwani? ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, wakinena, Asulibiwe.


akinena, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na khatiya. Wakanena, Bassi, haya yatukhussu nini sisi? Tazama wewe hayo.


Bassi yule akida, nao walio pamoja nae wakimwangalia Yesu, walipoliona tetemeko la inchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakinena, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.


Ndipo likatimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema, Wakavitwaa vipande thelathini vya fedha, kima chake aliyetiwa kima, ambae watu miongoni mwa wana wa Israeli walimtia kima;


Simon Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hatta mikono yangu na kichwa changu pia.


Pilato akatokea tena nje akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa sioni khatiya yo yote kwake.


Ninyi mlimkana yule Mtakatifu, yule Mwenye haki, mkataka mpewe muuaji:


Maana alimfanya yeye asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili vefu, illi sisi tuwe haki ya Mungu katika Yeye.


Kwa maana Kristo nae aliteswa marra moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio baki, illi atulete kwa Mungu; mwili wake akifishwa, bali roho yake akihuishwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo