Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 27:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa liwali Pontio Pilato.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Wakamfunga pingu, wakamchukua, wakamkabidhi kwa Pilato, mkuu wa mkoa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Wakamfunga pingu, wakamchukua, wakamkabidhi kwa Pilato, mkuu wa mkoa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Wakamfunga pingu, wakamchukua, wakamkabidhi kwa Pilato, mkuu wa mkoa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Wakamfunga, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato, aliyekuwa mtawala Mrumi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Wakamfunga, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato, ambaye alikuwa mtawala wa Kirumi.

Tazama sura Nakili




Mathayo 27:2
25 Marejeleo ya Msalaba  

na watampeleka kwa Mataifa wapate kumdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumsulibi; na siku ya tatu atafufuka.


Na jambo hili likisikilikana kwa liwali, tutasema nae, nanyi tutawaondoa shaka.


WAKATI huohuo walikuwapo watu wakimwarifu khabari za Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.


Wakamvizia wakatuma wapelelezi, nao wakajifanya kuwa wenye haki, illi wamnase kwa neno lake, kusudi wamtie katika enzi na mamlaka ya liwali.


WAKAONDOKA jamii yote, wakamleta kwa Pilato.


Ndipo Herode na Pilato wakapatana, siku ileile; kwa maana kwanza walikuwa na uadui wao kwa wao.


HATTA katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Tiberio Kaisari, Pontio Pilato alipokuwa liwali wa Yahudi, na Herode tetrarka wa Galilaya, na Filipo ndugu yake tetrarka wa Iturea, na wa inchi ya Trakoniti, na Lusania tetrarka wa Abilene,


Bassi kile kikosi na yule jemadari na wale watumishi wa Wayahudi wakamkamata Yesu, wakanifunga,


Bassi Anna akampeleka amefungwa kwa Kayafa kuhani mkuu.


Bassi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa hatta Praitorio; ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya Praitorio, wasije wakatiwa najis, bali waile Pasaka.


Hatta wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku uleule. Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili: walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza.


Kiisha jemadari akakaribia, akamshika, akaamuru afungwe kwa minyororo miwili: akauliza, Nani huyu? tena, amefanya nini?


Hatta walipokwisha kumfunga kwa kamba, Paolo akamwambia akida aliyesimama karibu, Je! ni halali kumpiga mtu Mrumi nae hajahukumiwa bado?


Bassi wale waliokuwa tayari kumwuliza wakaondoka wakamwacha. Na yule jemadari nae akaogopa, alipojua ya kuwa ni Mrumi, na kwa sababu amemfunga.


Na miaka miwili ilipotimia. Feliki akampokea Porkio Festo atawale badala yake. Na Feliki, akitaka kuwafanyia Wayahudi fadhili, akamwacha Paolo amefungwa.


Bassi kwa ajili ya hayo, nimewaiteni mje kunitazama na kusema nami; kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli.


Mungu wa Ibrahimu na Isaak na Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambae ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe.


Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika juu ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,


akataka ampe khati za kwenda Dameski zilizoandikwa kwa masunagogi, illi akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemi.


Nakuagiza mbele za Mungu avipae vitu vyote uzima, na mbele za Kristo Yesu aliyeungama maungamo yale mazuri mbele ya Pontio Pilato,


Katika huyu nimeteswa kiasi cha kufungwa, kama mtenda mabaya; illakini neno la Mungu halifungwi.


Wakumbukeni waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao; nao wanaodhulumiwa, kwa kuwa nanyi m katika mwili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo