Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 27:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 ILIPOKUWA assubuhi, makuhani wakuu wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumfisha;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Kulipopambazuka, makuhani wakuu wote na wazee wa watu walifanya mashauri juu ya Yesu wapate kumuua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Kulipopambazuka, makuhani wakuu wote na wazee wa watu walifanya mashauri juu ya Yesu wapate kumuua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Kulipopambazuka, makuhani wakuu wote na wazee wa watu walifanya mashauri juu ya Yesu wapate kumuua.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri pamoja dhidi ya Isa ili kumuua.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri pamoja dhidi ya Isa ili kumuua.

Tazama sura Nakili

Mathayo 27:1
16 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wenu waandisbi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapokea hukumu iliyo kubwa mno.

MARRA ilipokuwa assubuhi makuhani wakuu wakafanya shauri pamoja na wazee na waandishi na haraza zima, wakamfunga Yesu, wakamchukua, wakamleta kwa Pilato.

WAKATI huohuo walikuwapo watu wakimwarifu khabari za Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.

Hatta ulipokuwa mchana wakakusanyika jamii ya wazee wa watu, na makuhani wakuu, na waandishi, wakamleta kwa haraza yao, wakisema,

Bassi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa hatta Praitorio; ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya Praitorio, wasije wakatiwa najis, bali waile Pasaka.

Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja kuhani mkuu nao walio pamoja nae, wakawaita watu wa haraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani illi wawalete.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo