Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 26:56 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

56 Lakini jambo hili lote limekuwa, illi maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

56 Lakini haya yote yametendeka ili maandiko ya manabii yatimie.” Kisha wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

56 Lakini haya yote yametendeka ili maandiko ya manabii yatimie.” Kisha wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

56 Lakini haya yote yametendeka ili maandiko ya manabii yatimie.” Kisha wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

56 Lakini haya yote yametukia ili maandiko ya manabii yapate kutimia.” Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha na kukimbia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

56 Lakini haya yote yametukia ili maandiko ya manabii yapate kutimia.” Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha na kukimbia.

Tazama sura Nakili




Mathayo 26:56
17 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hili lilikuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?


Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa: lakini ole wake mtu yule ambae Mwana wa Adamu anasalitiwa nae! Ingekuwa kheri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.


Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu: kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchunga, na kondoo wa kundi watatawanyika.


Yatatimizwaje bassi maandiko, kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kuwa?


Saa inakuja, naam, imekwisha kuja, mtatawanyika killa mmoja kwa mambo yake, mtaniacha mimi peke yangu; wala mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.


Ndugu imepasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daud, katika khabari za Yuda, aliyekuwa kiongozi wao waliomkamata Yesu: kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi,


mtu huyu alitwaliwa nanyi kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake taugu zamani, nanyi mkamsulibisha kwa mikono mibaya, mkamwua:


Katika jawabu yangu ya kwauza hakuna mtu aliyesimama pamoja nami, bali wote waliniacha; wasihesabiwe khatiya kwa jambo bili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo