Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 26:41 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

41 Kesheni, kaombeni, msije mkaingia majaribuni: Roho ina nia njema, bali mwili ni dhaifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

41 Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho inataka lakini mwili ni dhaifu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

41 Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho inataka lakini mwili ni dhaifu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

41 Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho inataka lakini mwili ni dhaifu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

41 Kesheni na mwombe, msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi, lakini mwili ni mdhaifu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

41 Kesheni na mwombe, msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi, lakini mwili ni mdhaifu.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 26:41
34 Marejeleo ya Msalaba  

Kesheni bassi: kwa maana hamwijui saa atakayokuja Bwana wenu.


Bassi kesheni, maana hamwijui siku wala saa ajapo Mwana wa Adamu.


Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkakeshe pamoja nami.


Usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu.


Kesheni, kasalini, msipate kuingia majaribuni: roho ina nia njema, hali mwili dhaifu.


Utupe leo riziki zetu. Utusamehe dhambi zetu, kwa maana sisi nasi tunamsamehe killa mtu anaewiwa nasi. Usituingize majaribuni, hali utuokoe na yule mwovu.


Kwa hiyo kesheni killa wakati, mkiomba mpate kuhesabiwa kuwa mmestahili kuponea haya yote yatakayokuwa, na kusimama mahali penu mbele ya Mwana wa Adamu.


Alipofika pahali pale, akawaambia, Ombeni, msiingie majaribuni.


Mbona mnielala? Ondokeni, mkaombe, msipate kuingia majaribuni.


Na wale juu ya mwamba ndio wale ambao, walisikiapo neno, hulipokea kwa furaha; na hawa hawana mizizi, huamini kwa kitambo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.


Maana yale yasiyowezekana kwa sharia, kwa kuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa ajili ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili:


Jaribu halikuwapata ninyi, illa ya kadiri ya kibinadamu; na Mungu yu amini; hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, illi mweze kustahimili.


Kesheni, simameni imara katika Imani, mwe waume, mwe hodari.


bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwakhubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.


Nao walio watu wa Kristo Yesu wameusulibisha niwili pamoja na mawazo mabaya na tamaa mbaya.


kwa sala zote na kuomha mkisali killa wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo, mkifanya juhudi sana, na kuwaombea watakatifu wote,


Mwisho wa mamho yote umekaribia; bassi, mwe na akili, mkakeshe katika sala:


Erevukeni, kesheni; kwa kuwa mshitaki wenu Shetani, kama simba angurumae, huzungukazunguka, akitafuta mtu amle;


Bwana ajua kuwaokoa wamchao na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hatta siku ya hukumu;


Tazama, naja kama mwizi. Yu kheri akeshae, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi wakaone aibu yake.


Kwa kuwa ulilishika neno la uvumilivu wangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya inchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo