Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 26:36 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

36 Kiisha Yesu akaenda pamoja nao hatta kiwanja kiitwacho Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa, hatta niende kule nikasali.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

36 Kisha Yesu akaenda pamoja nao bustanini Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa nami niende pale mbele kusali.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

36 Kisha Yesu akaenda pamoja nao bustanini Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa nami niende pale mbele kusali.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

36 Kisha Yesu akaenda pamoja nao bustanini Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa nami niende pale mbele kusali.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

36 Kisha Isa akaenda pamoja na wanafunzi wake hadi kwenye bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia, “Kaeni hapa, nami niende kule nikaombe.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

36 Kisha Isa akaenda pamoja na wanafunzi wake mpaka kwenye bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia, “Kaeni hapa, nami niende kule nikaombe.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 26:36
10 Marejeleo ya Msalaba  

Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akiomba, akinena, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kinipitie; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.


Akaenda tena marra ya pili, akaomba, akinena, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kinipitie nisipokinywa, bassi, mapenzi yako yafanyike.


Bali wewe usalipo, ingia chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele ya Baba yako aliye kwa siri: na Baba yako aonae kwa siri atakujazi kwa dhahiri.


Yeye siku hizo za niwili wake alimtolea yeye awezae kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa sababu ya kicho chake;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo