Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 24:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Wakati huo watawasaliti ninyi mpate kuteswa, na watawaua; na mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa vote kwa ajili ya jina langu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 “Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa sababu ya jina langu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 “Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa sababu ya jina langu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 “Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa sababu ya jina langu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 “Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 “Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 24:9
26 Marejeleo ya Msalaba  

nao waliosalia wakawakamata watumishi wake, wakawatenda jeuri, wakawana.


Kwa sababu hii, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi: na wengine wao mtawaua na mtawasulibi, na wengine wao mtawapiga katika sunagogi zenu, na mtawafukuza mji kwa mji;


Na kwa hiyo hekima ya Mungu ilisema, Nitatuma kwao manabii na mitume, na wataua baadhi yao, na kuwaudhi,


Lakini kabla ya haya yote watawakamateni na kuwaudhini, watawapelekeni mbele ya sunagogi na gerezani, mkichukuliwa mbele ya wafalme na maliwali kwa ajili ya jina langu.


Ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi.


Lakini haya yote watawatenda kwa sababu ya jina langu, kwa kuwa hawamjui aliyenipeleka.


Watawaharamisha masunagogi: naam, saa inakuja, atakapodhani killa mtu awauae kuwa amtolea Mungu ibada.


Lakini tunataka kusikia kwako uonavyo wewe; kwa maana katika khabari za madhehebu hiyo tumekwisha kujua kwamba inanenwa vibaya kilia mahali.


Wakampiga mawe Stefano, nae akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu.


Illakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hili.


Usiogope mambo yatakavokupata: tazama mshitaki atawatupa baadhi yenu gerezani illi mjaribiwe, nanyi mtakuwa na mateso siku kumi. Uwe mwaminifu hatta kufa, nami nitakupa taji ya uzima.


Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha Shetani: nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hatta katika siku za Antipa shahidi wangu mwaminifu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.


Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hawo ndio wanaotoka katika shidda ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao wakayafanya meupe katika damu ya Mwana Kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo