Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 24:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwako na njaa, na maradhi, na matetemeko ya inchi pahali pahali.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali.

Tazama sura Nakili

Mathayo 24:7
20 Marejeleo ya Msalaba  

kutakuwa na matetemeko makubwa ya inchi mahali mahali, na njaa, na tauni. Kutakuwa na mambo ya kutisha, na ishara kuu kutoka mbinguni.

Akasimama mmojawapo wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa nweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima; nayo ikatukia katika siku za Klaudio Kaisari.

Nitatoa ajabu katika mbingu juu, Na ishara katika inchi chini, Damu na moto, na mvuke wa moshi:

Neno lile, Marra moja tena, ladhihirisha kuhamishwa vile viwezavyo kutetemeshwa, kama vitu vilivyoumbwa, illi vitu visivyoweza kutetemeshwa vikae.

Nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, tazama, palikuwa tetemeko kuu la inchi, jua likawa jeusi kama gunia la nywele, mwezi ukawa kama damu,

Na alipoifungua muhuri ya tatu nikamsikia nyama wa tatu mwenye uhayi akisema, Njoo, none. Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake.

Nikasikia sauti kati kati ya nyama wane wenye uhayi, ikisema, Kibaba cha nganu kwa nussu rupia, na vibaba vitatu vya shairi kwa nussu rupia, wala usiyadhuru mafuta na mvinyo.

Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Manti, na Kuzimu akafuatana nae. Wakapewa mamlaka juu ya robo ya inchi wane kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa nyama mwitu wa inchi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo