Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 24:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Hatta alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakinena, Tuambie, haya yatakuwa lini? Na nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni, wanafunzi walimwendea faraghani, wakamwuliza, “Tuambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonesha kuja kwako na mwisho wa nyakati?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni, wanafunzi walimwendea faraghani, wakamwuliza, “Tuambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonesha kuja kwako na mwisho wa nyakati?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni, wanafunzi walimwendea faraghani, wakamwuliza, “Tuambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonesha kuja kwako na mwisho wa nyakati?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Isa alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamjia faraghani, wakamuuliza, “Tuambie, mambo haya yatatukia lini, nayo dalili ya kuja kwako na ya mwisho wa dunia ni gani?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Isa alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamjia faraghani, wakamuuliza, “Tuambie, mambo haya yatatukia lini, nayo dalili ya kuja kwako na ya mwisho wa dunia ni gani?”

Tazama sura Nakili

Mathayo 24:3
23 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha Yesu akawaacha makutano, akaingia nyumbani: wanafunzi wake wakamwendea, wakinena, Tufafanulie mfano wa magugu ya konde.

Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia: malaika watatokea, watawatenga waovu na wenye haki,

Ndipo wanafunzi wake wakamwendea, wakamwambia, Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile walichukizwa?

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.

Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawo wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hatta watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.

Kiisha wale wanafunzi wakaniwendea Yesu kwa feragha, wakasema, Mbona sisi hatukuweza kumfukuza?

HATTA walipokaribia Yerusalemi, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu akatuma wanafunzi wawili,

Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hatta magharibi; hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni: ndipo mataifa yote ya ulimwengu wataomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbingu kwa nguvu pamoja na utukufu mwingi.

Lakini kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo na kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

wasitambue, hatta gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo na kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angalijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa.

mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi: nti tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hatta mwisho wa dunia. Amin.

Wakuimwuliza, wakisema, Mwalimu, haya yatakuwa lini, bassi? Na nini dalili ya kuwa haya yote ni karibu ya kutimia?

Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.

kana ni hivyo, ingalimpasa kuteswa marra nyingi tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu; lakini sasa, marra moja tu, katika mwisho wa dunia, ameonekana, atangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo