Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 24:27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

27 Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hatta magharibi; hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 maana, kama vile umeme uangazavyo toka mashariki hadi magharibi, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 maana, kama vile umeme uangazavyo toka mashariki hadi magharibi, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 maana, kama vile umeme uangazavyo toka mashariki hadi magharibi, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Kwa maana kama vile radi itokavyo mashariki na kuonekana hata magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Kwa maana kama vile umeme utokeavyo mashariki na kuonekana hata magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 24:27
18 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.


Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawo wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hatta watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.


Bassi wakiwaamhieni, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.


Hatta alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakinena, Tuambie, haya yatakuwa lini? Na nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?


Lakini kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo na kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.


wasitambue, hatta gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo na kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.


Kwa sababu hii na ninyi mwe tayari; kwa sababu saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.


Yesu akamwambia, Mbweha wana matundu, na ndege za anga vituo; bali Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.


Bassi, na ninyi subirini, jithubutisheni mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia.


na kusema, iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali hiyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo