Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 24:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Kwa maana wataondoka Makristo ya uwongo, na manabii ya uwongo, nao watafanyiza ishara kubwa ua mataajabu; wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wateule.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Maana watatokea akina Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Watafanya ishara kubwa na maajabu ya kuweza kuwapotosha ikiwezekana hata wateule wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Maana watatokea akina Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Watafanya ishara kubwa na maajabu ya kuweza kuwapotosha ikiwezekana hata wateule wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Maana watatokea akina Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Watafanya ishara kubwa na maajabu ya kuweza kuwapotosha ikiwezekana hata wateule wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Kwa maana watatokea masihi wa uongo na manabii wa uongo, nao watafanya ishara kubwa na maajabu mengi ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata wale wateule hasa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Kwa maana watatokea masihi wa uongo na manabii wa uongo, nao watafanya ishara kubwa na maajabu mengi ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata wale wateule hasa.

Tazama sura Nakili




Mathayo 24:24
31 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana wengi waitwao, wateule wachache.


Na manabii wengi wa uwongo wataondoka, watadanganya wengi.


Na kama siku zile zisingalikatizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitakatizwa siku zile.


Angalieni, nimetangulia kuwaambieni.


Nae atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya panda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande mmoja wa mwisho wa mbinguni mpaka upande wa pili.


Kwa maana wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, Mimi ni Kristo; na watadanganya wengi.


Jihadharini na manabii wa uwongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa wa mwitu wakali.


kwa maana wataondoka Makristo wa nwongo, na manabii wa uwongo, watatoa ishara na ajabu, wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wale wateule.


Bassi Mungu je! hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, nae ni mvumilivu kwao? Nawaambieni atawapatia haki upesi.


Bassi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa.


Yote anipayo Bwana itakuja kwangu; nae ajae kwangu sitamtupa nje kamwe.


Na mapenzi yake Baba aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika vyote alivyonipa nisipoteze kitu hatta kimoja, hali nikifufue siku ya mwisho.


Kwa sababu Paolo amekusudia kupita Efeso merikebuni, asije akakawia katika Asia: kwa maana alikuwa akifanya haraka, akitaka kuwahi Yerusalemi siku ya Pentekote, kama ikiwezekana.


Kama yumkini, kwa upande wenu, mwe na amani na watu wote.


Ku wapi, bassi, kule kujiita kheri? Maana nawashuhudia, kwamba, kama ingaliwezekana, mngaliugʼoa macho yenu, mkanipa mimi.


Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake; tena, killa alilajae jina la Bwana na aache uovu.


mnaolindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani mpate wokofu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.


Bassi, wapenzi, mkitangulla kujua haya, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hawo wakhalifu, mkaanguka na kuuacha uthubutifu wenu.


Watoto, ni wakati wa mwisho: na kama vile mlivyosikia kwamba adui wa Kristo yuaja, hatta sasa adui wengi wa Kristo wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.


Naui aliye mwongo illa yeye akanae ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye adui wa Kristo, amkanae Baba na Mwana.


Twajua ya kuwa killa mtu aliyezaliwa na Mungu hakosi: bali yeye aliyezaliwa na Mungu ajilinda, na yule mwovu hamgusi.


Yule nyama akakamatwa, na nabii wa uwongo aliye pamoja nae, yeye aliyezifanya ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile alama ya nyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa hayi katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo