Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 23:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnalipa zaka za mnaana na bizari na kumini, mkaacha mambo makuu ya sharia, hukumu, na rehema, na imani: haya imewapasa kuyafanya, na mengine yale msiyaache.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnatoza watu sehemu moja ya kumi, hata juu ya majani yenye harufu nzuri, bizari na jira, na huku mnaacha mambo muhimu ya sheria kama vile haki, huruma na imani. Haya ndio hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnatoza watu sehemu moja ya kumi, hata juu ya majani yenye harufu nzuri, bizari na jira, na huku mnaacha mambo muhimu ya sheria kama vile haki, huruma na imani. Haya ndio hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 “Ole wenu walimu wa Torati na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnatoa zaka ya mnanaa, bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu zaidi ya sheria, yaani haki, huruma na uaminifu. Iliwapasa kufanya haya makuu ya sheria bila kupuuza hayo matoleo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

Mathayo 23:23
16 Marejeleo ya Msalaba  

Kama mngalijua maana ya maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, hamngaliwalaumu wasio na khatiya.

Ole wenu waandisbi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapokea hukumu iliyo kubwa mno.

Lakini shikeni njia, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka: kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.

Bali ole wenu Mafarisayo, kwa sababu mnalipa zaka za mnaana na mchicha, na killa mboga, mkaacha adili na upendo wa Mungu: iliwapaseni kuyafanya haya ya kwanza bila kuacha haya ya pili.

Nafunga marra mbili kwa juma; nalipa zaka za mapato yangu yote.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo