Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 23:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnazunguka katika bahari na inchi kavu illi kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehannum marra mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 “Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumpata mtu mmoja afuate dini yenu. Mnapompata, mnamfanya astahili maradufu kwenda katika moto wa Jehanamu kuliko nyinyi wenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 “Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumpata mtu mmoja afuate dini yenu. Mnapompata, mnamfanya astahili maradufu kwenda katika moto wa Jehanamu kuliko nyinyi wenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 “Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumpata mtu mmoja afuate dini yenu. Mnapompata, mnamfanya astahili maradufu kwenda katika moto wa Jehanamu kuliko nyinyi wenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 “Ole wenu walimu wa Torati na Mafarisayo, enyi wanafiki! Ninyi mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja mwongofu, lakini baada ya kumpata, mnamfanya mwana wa Jehanamu mara mbili kuliko ninyi!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 “Ole wenu walimu wa Torati na Mafarisayo, enyi wanafiki! Ninyi mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja mwongofu, lakini baada ya kumpata, mnamfanya mwana wa Jehanamu mara mbili kuliko ninyi!

Tazama sura Nakili

Mathayo 23:15
17 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wenu waandisbi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapokea hukumu iliyo kubwa mno.

Hatta akiona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, akawaambia, Uzao wa nyoka, nani aliyewaonya mkimbie ghadhabu ijayo?

Bali mimi nawaambiem, Killa amwoneae ndugu yake ghadhabu bila sababu, itampasa hukumu; na mtu akimwambia ndugu yake, Haka, itampasa baraza; na mtu akinena, Mpumbavu, itampasa jebannum ya moto.

Jicho lako la kuume likikukosesha, lingʼoe ulitupe mbali nawe: kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehannum.

Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo.

Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa shetani, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?

Sunagogi lilipofumukana, Wayahudi wengi na waongofu watawa wakashikamana na Paolo na Barnaba; nao, wakisema nao, wakawatia moyo kudumu katika neema ya Mungu.

Wayahudi wakalika toka Antiokia na Ikonio, wakawashawishi makutano hatta wakampiga mawe Paolo wakamhurura nje ya mji, wakidhani ya kuwa amekwisha kufa.

Walakini Wayahudi wasioamini wakawataharakisha watu wa mataifa na kuwatia nia mbaya juu ya ndugu.

Lakini Wayahudi wa Thessaloniki walipopata khabari ya kwamba Neno la Mungu linakhubiriwa na Paolo katika Beroya, wakaenda huko wakawachafua makutano.

Frugia na Pamfulia, Misri na pande za Libua karibu na Kurene, na Warumi wageni, Wayahudi na Waongofu,

Neno hili likapendeza machoni jia mkutano wote: wakamehagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu na Filipo, na Prokoro, na Nikanor, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia.

Wao wawaonea uinyi shauku lakini si kwa vema bali wanataka kuwafungia mlango illi ninyi mwaonee wao shauku.

Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mwili, ndio wanaokushurutisheni kutahiriwa: wasiudhiwe tu kwa ajili ya msalaba wa Kristo.

ambazo sisi nasi sote tuliziendea, hapo zamani, katika tamaa za mwili wetu, tukiyatimiza mapenzi ya mwili wetu na ya nia zetu, tukawa kwa tabia yetu watoto wa ghadhabu kama na hao wengine.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo