Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 22:44 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

44 Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti mkono wangu wa kuume, Hatta niwawekapo adui zako chini ya miguu yako?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

44 ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

44 ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

44 ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

44 “ ‘Mwenyezi Mungu alimwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.”’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

44 “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.” ’

Tazama sura Nakili




Mathayo 22:44
20 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, Daud akimwita Bwana, amekuwaje mwana wake?


Yesu akamwambia. Wewe umesema: lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwoua Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu.


Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.


Walakini wale adui zangu wasiotaka niwatawale, waleteni huku mkawachinje mhele zangu.


Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu, na Mungu wangu.


kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, lililotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo killa mahali, Bwana wao na wetu:


Maana sharti amiliki yeye, hatta awaweke maadui wote chini ya miguu yake.


Naam, naliona mambo yote kuwa khasara kwa ajili ya uzuri usio kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambae kwa ajili yake nimepata khasara ya mambo yote, nikiyahesabu kuwa kania mavi illi nimpate Kristo;


Je! yuko malaika aliyeambiwa nae maneno haya wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume hatta nitakapoweka adui zako chiui ya nyayo zako?


Yeye kwa kuwa ni mwanga wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivitengeneza vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya peke yake utakaso wa dhambi zetu, aliketi juu mkono wa kuume wa ukuu;


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


Nikamwonu nyama, na wafalme wa inchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, na na majeshi yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo