Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 22:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 wakinena, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, nae hana watoto, ndugu yake amwoe mkewe, illi ampatie ndugu yake mzao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Basi, wakamwambia, “Mwalimu, Mose alisema mtu aliyeoa akifa bila kuacha watoto, lazima ndugu yake amwoe huyo mama mjane, ili ampatie ndugu yake watoto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Basi, wakamwambia, “Mwalimu, Mose alisema mtu aliyeoa akifa bila kuacha watoto, lazima ndugu yake amwoe huyo mama mjane, ili ampatie ndugu yake watoto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Basi, wakamwambia, “Mwalimu, Mose alisema mtu aliyeoa akifa bila kuacha watoto, lazima ndugu yake amwoe huyo mama mjane, ili ampatie ndugu yake watoto.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 “Mwalimu, Musa alisema, ‘Mtu akifa bila kuwa na watoto, ndugu yake inampasa amwoe huyo mjane ili ampatie watoto huyo nduguye aliyekufa.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 “Mwalimu, Musa alisema, ‘Kama mtu akifa bila kuwa na watoto, ndugu yake inampasa amwoe huyo mjane ili ampatie watoto huyo nduguye aliyekufa.’

Tazama sura Nakili




Mathayo 22:24
14 Marejeleo ya Msalaba  

Wakawatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodiano, wakanena, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, ua njia va Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu, kwa maana hutazami sura za watu.


Bassi, kwetu palikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia ndugu yake nike wake.


Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?


Siye killa mtu aniambiae, Bwana, Bwana, atakaeingia katika ufalme wa mbinguni; hali yeye afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.


wakamwuliza wakinena, Mwalimu, Musa alituandikia ya kwamba ndugu ya mtu akifa, akamwacha mke wake wala hana mtoto, ndugu yake amtwae yule mke wake akampatie ndugu yake mzao.


Mwalimu, Musa alituandikia ya kama ndugu ya mtu akifa, nae ana mke, na mtu huyo akifa hana mtoto, ni lazima ndugu yake amtwae yule mke, akampatie ndugu yake mzao.


Bassi katika kiyama, atakuwa mke wa nani katika hawo? maana wale saba walikuwa nae.


Ya nini kuniita Bwana, Bwana, nanyi hamyatendi niyanenayo?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo