Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 22:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Wakawatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodiano, wakanena, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, ua njia va Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu, kwa maana hutazami sura za watu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Basi, wakawatuma wafuasi wao pamoja na wafuasi wa kikundi cha Herode. Wakamwuliza, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu, na kwamba wafundisha njia ya Mungu kwa uaminifu; humwogopi mtu yeyote, maana cheo cha mtu si kitu kwako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Basi, wakawatuma wafuasi wao pamoja na wafuasi wa kikundi cha Herode. Wakamwuliza, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu, na kwamba wafundisha njia ya Mungu kwa uaminifu; humwogopi mtu yeyote, maana cheo cha mtu si kitu kwako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Basi, wakawatuma wafuasi wao pamoja na wafuasi wa kikundi cha Herode. Wakamwuliza, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu, na kwamba wafundisha njia ya Mungu kwa uaminifu; humwogopi mtu yeyote, maana cheo cha mtu si kitu kwako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Wakatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode kwake. Nao wakasema, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu na unafundisha njia ya Mungu katika kweli bila kuyumbishwa na mtu wala kuonesha upendeleo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Wakatuma wanafunzi wao kwake pamoja na Maherode. Nao wakasema, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu na unafundisha njia ya Mungu katika kweli bila kuyumbishwa na mtu wala kuonyesha upendeleo.

Tazama sura Nakili




Mathayo 22:16
36 Marejeleo ya Msalaba  

wakinena, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, nae hana watoto, ndugu yake amwoe mkewe, illi ampatie ndugu yake mzao.


Vivyo hivyo wa pili nae, na wa tatu, hatta wote saba.


Akasema, Enendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie, Mwalimu anena, Majira yaugu i karibu; kwako nitafanya pasaka pamoja na wanafunzi wangu.


Marra akamwendea Yesu, akasema, Salam, Rabbi, akambusu sana.


Hatta alipokuwa akitoka kwenda njiani mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanyeni nipate kuurithi uzima wa milele?


Wakatuma kwake baadhi ya Mafarisayo na Maherodiano, illi wamnase kwa maneno.


Hatta walipofika wakamwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu: lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! ni halali kumpa Kaisari kodi au sivyo? Tumpe, tusimpe?


marra wakaloka wale Mafarisayo, wakamfanyia shauri pamoja na Maherodiano jinsi ya kumwangamiza.


Akawaagiza, akisema, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode.


Wakamwuliza, wakinena, Mwalimu, twajua ya kuwa wanena yaliyo kweli na kuyafundisha, wala hujali cheo cha mtu, bali katika kweli waifundisha njia ya Mungu:


Yesu akajibu akamwambia, Simon, nina neno la kukuambia. Akanena, Mwalimu, sema.


Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.


Bassi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme bassi? Yesu akajibu, Wewe wanena ya kwamba mimi ni mfalme. Mimi nalizaliwa kwa ajili ya haya na kwa ajili ya haya nalikuja ulimwenguni, illi niishuhudie kweli. Killa aliye wa kweli hunisikia sauti yangu.


Yeye anenae kwa nafsi yake tu, hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anaetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyu ni wa kweli wala ndani yake hamna udhalimu.


Kwa maana sisi si kama wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama watu wasemao kwa weupe wa moyo, kaina watu watumwao na Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.


lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyosetirika, wala hatuenendi kwa ujanja, wala kulichanganya neno la Mungu na uwongo; hali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mhele za Mungu.


Hatta imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awae yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemjua Kristo kwa jinsi ya mwili, sasa lakini hatumjui hivi tena.


Maana sasa je! nawashawishi wana Adamu au Mungu? au nataka kuwapendeza wana Adamu? Kama ningekuwa hatta sasa nawapendeza wana Adamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.


Lakini wale wenye sifa kwamba wana cheo, walivyo vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwana Adamu—nasema, wale wenye sifa hawakuniongezea kitu,


bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuaminiwe Injili ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wana Adamu bali Mungu anaetupima mioyo yetu.


Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole,, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina wala unafiki;


Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo