Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 21:41 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

41 Wakamwambia, Atawaangamiza wabaya wale; nae atawapangisha mizabibu wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

41 Wao wakamjibu, “Atawaangamiza vibaya hao waovu, na lile shamba atawapa wakulima wengine ambao watampa sehemu ya mavuno wakati wake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

41 Wao wakamjibu, “Atawaangamiza vibaya hao waovu, na lile shamba atawapa wakulima wengine ambao watampa sehemu ya mavuno wakati wake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

41 Wao wakamjibu, “Atawaangamiza vibaya hao waovu, na lile shamba atawapa wakulima wengine ambao watampa sehemu ya mavuno wakati wake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

41 Wakamjibu, “Kwa hasira kuu, atawaangamiza kabisa hao wadhalimu na kulipangisha shamba lake la mizabibu kwa wakulima wengine ambao watampatia fungu lake la matunda wakati wa mavuno.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

41 Wakamjibu, “Kwa huzuni kuu atawaangamiza kabisa hao wadhalimu na kulipangisha shamba lake la mizabibu kwa wakulima wengine ambao watampatia fungu lake la matunda wakati wa mavuno.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 21:41
38 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumishi wake kwa wale wakulima, wajiokee matunda yake.


Bassi atakapokuja yule bwana wa mizabibu, atawatendea nini wale wakulima?


Kwa sababu hii nawaambieni, ya kwamba ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, na watapewa taifa lingine wenye kuzaa matunda yake.


Pepeto lake li mkononi mwake, nae ataitakasa sana sakafu yake; atakusanya nganu yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.


Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine.


Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwetu mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini.


Walipopingamana nae na kutukana, akakungʼuta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu: mimi ni safi: langu sasa nitakwenda kwa watu wa mataifa.


Bassi ijulikane kwenu ya kwamba wokofu huu wa Mungu umepelekwa kwa mataifa, nao watasikia.


Ikawa baba yake Publio alikuwa hawezi homa na kuhara damu. Paolo akaingia kwake, akaomba, akaweka mikono yake juu yake, akamponya


wakituzuia tusiseme na mataifa wapate kuokolewa; illi watimize dhambi zao siku zote; lakini hasira imewafikia hatta mwisho.


Angalieni msimkatae yeye anenae. Maana ikiwa wale hawakuokoka waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya inchi, sembuse sisi tukijiepusha nae atuonyae kutoka mbinguni:


sisi je! tutapataje kujiponya, tusipotunza wokofu mkiju namna hii? ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kiisha nkathubutika kwetu na wale waliosikia;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo