Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 21:33 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

33 Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, nae alipanda mizabibu, akazungusha uzio, akachimba shimo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Yesu akasema, “Sikilizeni mfano mwingine. Mtu mmoja mwenye nyumba alilima shamba la mizabibu; akalizungushia ukuta, akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga humo mnara pia. Kisha akalikodisha kwa wakulima, akasafiri kwenda hadi nchi ya mbali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Yesu akasema, “Sikilizeni mfano mwingine. Mtu mmoja mwenye nyumba alilima shamba la mizabibu; akalizungushia ukuta, akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga humo mnara pia. Kisha akalikodisha kwa wakulima, akasafiri kwenda hadi nchi ya mbali.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 “Sikilizeni mfano mwingine: Kulikuwa na mtu mmoja mwenye shamba ambaye alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, akatengeneza shinikizo la kukamulia zabibu ndani yake, na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha hilo shamba la mizabibu kwa wakulima fulani, naye akaondoka, akasafiri hadi nchi nyingine.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 “Sikilizeni mfano mwingine: Kulikuwa na mtu mmoja mwenye shamba ambaye alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, akatengeneza shinikizo ndani yake na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha hilo shamba la mizabibu kwa wakulima fulani, naye akaondoka, akasafiri kwenda nchi nyingine.

Tazama sura Nakili

Mathayo 21:33
23 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi.

KWA maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba, aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu.

Mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na watoto wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo enenda kufanya kazi katika shamba langu la mizabibu.

Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa:

Ni kana kwamba mtu mwenye kusafiri, ameacha nyumba yake, amewapa amri watumwa wake, na killa mtu kazi yake, amemwamuru bawabu akeshe.

Bassi akasema, Mtu mmoja, mungwana, alisafiri kwenda inchi ya mbali illi kujipatia ufalme na kurejea.

MIMI ndimi niliye mzabibu wa kweli, na Baba yangu ni mkulima.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo