Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 21:31 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

31 Katika hawa wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya baba yake? Wakamwambia, Yule wa kwanza. Yesu akawaambia, Amin, nawaambieni, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Je, ni nani kati ya hawa wawili aliyetimiza matakwa ya baba yake?” Wakamjibu, “Yule mtoto wa kwanza.” Basi, Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, watozaushuru na waasherati wataingia katika ufalme wa Mungu kabla yenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Je, ni nani kati ya hawa wawili aliyetimiza matakwa ya baba yake?” Wakamjibu, “Yule mtoto wa kwanza.” Basi, Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, watozaushuru na waasherati wataingia katika ufalme wa Mungu kabla yenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Je, ni nani kati ya hawa wawili aliyetimiza matakwa ya baba yake?” Wakamjibu, “Yule mtoto wa kwanza.” Basi, Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, watozaushuru na waasherati wataingia katika ufalme wa Mungu kabla yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 “Ni yupi kati yao hao wawili aliyetimiza kile alichotaka baba yake?” Wakamjibu, “Ni yule wa kwanza.” Isa akawaambia, “Amin, amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanawatangulia kuingia katika ufalme wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 “Ni yupi kati yao hao wawili aliyetimiza kile alichotaka baba yake?” Wakamjibu, “Ni yule wa kwanza.” Isa akawaambia, “Amin, amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanawatangulia kuingia katika Ufalme wa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 21:31
26 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana ye yote atakaeyafanya mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.


akasema, Amin, nawaambieni, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kabisa katika ufalme wa mbinguni.


Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza wa mwisho: maana waitwao wengi, hali wateule wachache.


Akamwendea yule wa pili, akasema vilevile. Nae akajibu akasema, Nakwenda, Bwana: asiende.


Kwa maana, amin nawaambieni, Mpaka mbingu na inchi zitakapoondoka, yodi moja na nukta moja ya torati haitaondoka, mpaka yote yatimie.


Maana mkiwapenda wanaowapendani, mwapata thawabu gani? Hatta watoza ushuru, je, nao hawafanyi yayo hayo?


Tena usalipo, usiwe kama wanafiki: kwa maana wapenda kusali wakisimama katika sunagogi na katika pembe za njia, illi waonekane na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao.


Siye killa mtu aniambiae, Bwana, Bwana, atakaeingia katika ufalme wa mbinguni; hali yeye afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.


Yesu alipokuwa anaondoka kutoka huko akaona mtu amekeli fordhani, aitwae Mattayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata.


Kadhalika nawaambia ninyi, iko furaha mbele ya malaika zake Mungu kwa mwenye dhambi mmoja atubuye.


Akamwambia, Kwa kinywa chako nitakuhukumu, ee mtumishi mwovu wewe. Ulijua ya kuwa mimi mtu mgumu, naondoa nisichoweka, navuna nisichopanda;


Watu wote na watoza ushuru waliposikia wakampa Mungu haki, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana.


Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa marra ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.


Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.


Bassi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hauoni; bali sasa anawakhuhiri watu wote wa killa mahali watubu.


Twajua ya kuwa mambo yote yasemwayo na torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, illi killa kinywa kifumbwe, ulimwengu wote ukapasiwe na hukumu ya Mungu:


Sharia iliingia illi anguko lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;


Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wahesabuvyo kukawia, bali huvumilia kwenu, hapendi mtu aliye yote apotee, bali wote wafikilie toba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo