Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 21:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Makutano wakanena, Huyu ni Yesu, yule nabii wa Nazareti ya Galilaya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Watu katika ule umati wakasema, “Huyu ni nabii Yesu, kutoka Nazareti mji wa Galilaya.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Watu katika ule umati wakasema, “Huyu ni nabii Yesu, kutoka Nazareti mji wa Galilaya.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Watu katika ule umati wakasema, “Huyu ni nabii Yesu, kutoka Nazareti mji wa Galilaya.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Wale umati wa watu wakajibu, “Huyu ni Isa, yule nabii kutoka Nasiri ya Galilaya.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Ule umati wa watu ukajibu, “Huyu ni Isa, yule nabii kutoka Nasiri katika Galilaya.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 21:11
20 Marejeleo ya Msalaba  

akaenda, akakaa mji uliokwitwa Nazareti: illi litimie neno lililonenwa na manabii, Atakwitwa Mnazorayo.


Hatta alipoingia Yerusalenn, mji wote ukataharuki, nkinena, Ni nani huyu?


Na tukisema, Kwa wana Adamu; twaogopa makutano; maana watu wote wanaona ya kuwa Yohana ni nabii.


Nao walipotafuta kumkamata, wakawaogopa makutano, kwa maana walimwona kuwa nabii.


Wengine walinena, Huyu ni nabii au kama mmoja wa manabii.


Illakini imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa, kwa maana haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemi.


Akawaambia, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu Mnazareti, aliyekuwa mtu nabii mwenye nguvu kwa tendo na kwa neno mbele za Mungu na watu wote;


Khofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu: na Mungu amewajilia watu wake.


Yule Farisayo aliyemwalika, alipoona haya akasema kimoyomoyo, akinena, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angalimjua huyu ni nani! na ni mwanamke gani anaemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi.


Wakamwuliza, Nini bassi? U Eliya wewe? Akanena, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.


Wakamwuliza, wakimwambia, Mbona bassi wabatiza, kama wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?


Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii.


Bassi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya Yesu, wakasema, Huyu hakika ni nabii yule ajae ulimwenguni.


Bassi watu wengi katika makutano waliposikia neno lile, walinena, Huyu hakika yake ndiye nabii yule.


Kukawa matangukano kati yao. Bassi wakamwambia yule kipofu marra ya pili, Wewe unasema nini katika khabari zake kwa kuwa alikufumbua macho? Akasema, Yu nabii.


Musa huyo ndiye aliyewaambia wana wa Israeli, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii katika ndugu zenu, kama mimi: mtamsikia huyo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo