Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 20:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 Lakini kwemi ninyi haitakuwa hivi: bali ye yote atakae kuwa mkuu kwenu, na awe mkhudumu wenu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Lakini kwenu isiwe hivyo, ila anayetaka kuwa mkuu kati yenu sharti awe mtumishi wa wote;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Lakini kwenu isiwe hivyo, ila anayetaka kuwa mkuu kati yenu sharti awe mtumishi wa wote;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Lakini kwenu isiwe hivyo, ila anayetaka kuwa mkuu kati yenu sharti awe mtumishi wa wote;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkuu miongoni mwenu hana budi kuwa mtumishi wenu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkuu miongoni mwenu hana budi kuwa mtumishi wenu,

Tazama sura Nakili




Mathayo 20:26
23 Marejeleo ya Msalaba  

na ye yote atakae kuwa wa kwanza kwenu awe mtumishi wenu:


Ndipo hawo pia watajibu, wakinena, Bwana, lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikukhudumu?


Na palikuwa na wanawake wengi huko wakitazama kwa mbali, hawo ndio waliomfuata Yesu toka Galilaya, na kumtumikia.


Lakini haitakuwa hivi kwemi; bali mtu atakae kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mkhudumu wenu,


Kwa maana Mwana wa Adamu nae hakuja kukhudumiwa bali kukhudumu, na kutoa roho yake iwe dia ya wengi.


Akaketi chini akawaita wathenashara akawaambia, Mtu atakae kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mkhudumu wa wote.


Nawaambia ninyi, huyu alishuka nyumbani kwake amepata kibali kuliko yule: kwa maana killa ajikwezae atadhilika; nae ajidhiliye atakwezwa.


Lakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa wenu awe kama aliye mdogo; nafe atanguliae kama akhudumuye.


Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu, kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu: watumishi wangu wangalinipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi: lakini sasa ufalme wangu sio wa hapa.


Na walipokuwa katika Salamini wakalikhubiri neno la Bwana katika masunagogi ya Wayahudi, nao walikuwa nae Yohana kuwakhudumia.


Si kwamba tunatawala imani yenu; hali tu wasaidizi wa furaha yenu; maana mnasimama kwa imani.


Bwana na ampe kuona rehema kwa Bwana siku ile. Na jinsi alivyonikhudumia katika Efeso, wewe wajua sana.


ambae mimi nalimtaka akae nami, apate kunikhudumia hadala yako katika mafungo ya Injili;


Hawo wote si roho zitumikazo, wakitumwa kuwakhudumu wale watakaourithi wokofu?


Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akikhudumu, na akhudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; illi Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo; utukufu na uweza u kwake hatta milele na milele. Amin.


wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya mfano kwa lile kundi.


Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo