Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 20:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza hawa wanangu waketi mmoja mkono wako wa kunme; na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Yesu akamwuliza, “Unataka nini?” Huyo mama akamwambia, “Ahidi kwamba katika ufalme wako, hawa wanangu wawili watakaa mmoja upande wako wa kulia na mwingine upande wako wa kushoto.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Yesu akamwuliza, “Unataka nini?” Huyo mama akamwambia, “Ahidi kwamba katika ufalme wako, hawa wanangu wawili watakaa mmoja upande wako wa kulia na mwingine upande wako wa kushoto.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Yesu akamwuliza, “Unataka nini?” Huyo mama akamwambia, “Ahidi kwamba katika ufalme wako, hawa wanangu wawili watakaa mmoja upande wako wa kulia na mwingine upande wako wa kushoto.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Isa akamuuliza, “Unataka nini?” Akajibu, “Tafadhali, wajalie wanangu hawa ili mmoja aketi upande wako wa kuume, na mwingine upande wako wa kushoto katika ufalme wako.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Isa akamuuliza, “Unataka nini?” Akajibu, “Tafadhali, wajalie wanangu hawa ili mmoja aketi upande wako wa kuume, na mwingine upande wako wa kushoto katika Ufalme wako.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 20:21
24 Marejeleo ya Msalaba  

SAA ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakinena, Ni nani bassi aliye mkuu kafika ufalme wa mbinguni?


Yesu akamwambia, Amin, nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata, katika zamani za kuzaliwa upya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli.


Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomha. Mwaweza kuuywea kikombe nitakachonywea mimi, na kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi? Wakamwambia, Twaweza.


Yesu akasimama, akawaita, akasema, Mnataka niwafanyie nini?


Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyieni? Yule kipofu akamwambia, Rabbi, nipate kuona tena.


Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.


ndipo binti yake yule Herodias akaingia, akacheza, akampendeza Herode nao walioketi pamoja nae karamuni. Mfalme akamwambia yule kijana, Niombe lo lote utakalo, nitakupa.


na alipomkaribia akamwuliza, Wataka nikufanyie nini? Akasema, Bwami, nipate kuona.


Nao wakisikia haya akaongeza akawaambia mfano, kwa sababu alikuwa akikaribia Yerusalemi, nao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana marra moja.


Kulikuwa na mashindano kwao, ni nani anaehesabiwa kuwa mkubwa.


Mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, mtaomba killa mtakalo, na mtafanyiziwa.


Bassi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Bwana, wakati huu ndipo unapomrudishia Israeli ufalme wake?


Kwa pendo la udugu, mwe na shauku ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;


Ni nani atakaewahukumu? Kristo ndiye aliyekufa, naam, na zaidi ya haya, amefufuka, nae yuko mkono wa kuume wa Mungu, tena ndiye anaetuombea.


BASSI mkiwa mmefufuka panioja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko mkono wa kuume wa Mungu, ameketi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo