Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 20:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza wa mwisho: maana waitwao wengi, hali wateule wachache.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Yesu akamaliza kwa kusema, “Hivyo, walio wa mwisho watakuwa wa kwanza na wa kwanza watakuwa wa mwisho.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Yesu akamaliza kwa kusema, “Hivyo, walio wa mwisho watakuwa wa kwanza na wa kwanza watakuwa wa mwisho.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Yesu akamaliza kwa kusema, “Hivyo, walio wa mwisho watakuwa wa kwanza na wa kwanza watakuwa wa mwisho.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 “Vivyo hivyo, wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 “Vivyo hivyo, wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 20:16
18 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho, wa kwanza.


Katika hawa wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya baba yake? Wakamwambia, Yule wa kwanza. Yesu akawaambia, Amin, nawaambieni, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.


Kwa maana wengi waitwao, wateule wachache.


Ingieni kwa kupita mlango ulio mwembamba: maana ujia iendayo hatta upotevu ni pana, na mlango wake mpana, na wengi waingiao kwa mlango huo.


Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho: na wa mwisho wa kwanza.


Maana nawaambieni ya kwamba katika watu wale walioalikwa hapana hatta mmoja atakaeionja karamu yangu.


Nawaambieni, Kadhalika itakuwako furaha mbinguni kwa mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa wenye haki tissa na tissaini, wasiohitaji toba.


Kwa ajili hiyo, nakuambia, Amesamehewa dhambi zake zilizo nyingi kwa kuwa amependa sana. Nae asamehewae kidogo hupenda kidogo.


Sharia iliingia illi anguko lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;


Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hawa akawatukuza.


Tuseme nini, bassi? Ya kwamba watu wa mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; yaani ile haki iliyo ya imani;


Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa mlipopokea lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la kibinadamu; bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli, litendalo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo