Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 20:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 KWA maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba, aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 “Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu mwenye shamba la mizabibu, ambaye alitoka asubuhi na mapema kuwaajiri wafanyakazi katika shamba lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 “Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu mwenye shamba la mizabibu, ambaye alitoka asubuhi na mapema kuwaajiri wafanyakazi katika shamba lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 “Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu mwenye shamba la mizabibu, ambaye alitoka asubuhi na mapema kuwaajiri wafanyakazi katika shamba lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 “Kwa maana ufalme wa mbinguni unafanana na mtu mwenye shamba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri vibarua kufanya kazi katika shamba lake la mizabibu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 “Kwa maana Ufalme wa Mbinguni unafanana na mtu mwenye shamba aliyetoka alfajiri ili kwenda kuajiri vibarua kufanya kazi katika shamba lake la mizabibu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 20:1
22 Marejeleo ya Msalaba  

Akawatolea mfano mwingine, akinena, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake:


Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya kharadali, aliyotwati mtu akaipanda katika shamba lake;


Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke, akaisetiri katika pishi tatu za unga, hatta ukachacha wote pia.


Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya za killa namna:


Na alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, akawapeleka katika shamba lake la mizabibu.


Mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na watoto wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo enenda kufanya kazi katika shamba langu la mizabibu.


Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwana wake arusi.


Ee Yerusalemi, Yerusalemi, wenye kuwaua manabii, na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! marra ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkukubali!


NDIPO ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.


Maana ni mfano wa mtu atakae kusafiri kwenda inchi ya ugeni, aliwaita watumishi wake, akaweka kwao mali zake.


Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


Ni kana kwamba mtu mwenye kusafiri, ameacha nyumba yake, amewapa amri watumwa wake, na killa mtu kazi yake, amemwamuru bawabu akeshe.


MIMI ndimi niliye mzabibu wa kweli, na Baba yangu ni mkulima.


Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana.


awafanye kuwa wrakamilifu katika killa tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, nae akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo