Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 2:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Akakusanya makuhani wakuu wote na waandishi wa watu, akatafuta khabari kwao, Kristo azaliwa wapi?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Basi, akawaita pamoja makuhani wakuu wote na waalimu wa sheria, akawauliza, “Kristo atazaliwa wapi?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Basi, akawaita pamoja makuhani wakuu wote na waalimu wa sheria, akawauliza, “Kristo atazaliwa wapi?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Basi, akawaita pamoja makuhani wakuu wote na waalimu wa sheria, akawauliza, “Kristo atazaliwa wapi?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Herode akawaita pamoja viongozi wa makuhani na walimu wa Torati, akawauliza ni wapi ambapo Al-Masihi angezaliwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Herode akawaita pamoja viongozi wa makuhani na walimu wa Torati, akawauliza ni mahali gani ambapo Al-Masihi angezaliwa.

Tazama sura Nakili




Mathayo 2:4
30 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaambia, Kwa sababu hii, killa mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoae katika hazina yake vitu vipya na vya kale.


Mfalme Herode aliposikia haya, akafadhaika, na Yerusalemi pia pamoja nae.


Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Yahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,


Lakini makuhani wakuu na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto wakipaaza sauti zao hekaluni, wakinena, Utuokoe sasa, mwana wa Daud! wakakasirika,


Hatta alipokwisha kuingia hekaluni, makuhani wakuu na wazee wa watu wakamwendea alipokuwa akifundisha, wakinena, Kwa mamlaka gani unafanya haya? Na nani aliyekupa mamlaka haya?


Ndipo makubani wakuu, na waandishi, na wazee wa watu wakakusanyika katika behewa ya kuhani mkuu aliyeitwa Kayafa;


Hatta alipokuwa akisema, Yuda, mmoja wa wale thenashara akaja, na pamoja nae makutano mengi, wana panga na marungu, wametoka kwa makuhani wakuu na wazee wa watu.


ILIPOKUWA assubuhi, makuhani wakuu wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumfisha;


kwa maana alikuwa akiwafundisha kwa namna ya mwenye mamlaka, wala si kama waandishi wao.


Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na makuhani, wakuu na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka.


Makuhani wakuu na waandishi wakatafuta kumkamata saa hiyo hiyo, wakawaogopa watu: maana walitambua ya kuwa ule mfano amewanena wao.


Wakasimama makuliani wakuu na waandishi, wakimshitaki kwa nguvu.


Bassi Yuda akiisha kupokea kikosi cha askari, na watumishi waliotoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo, akaenda huko na makandili na taa za mkono na silaha.


Yesu akajibu akamwambia, Je! Wewe u mwalimu katika Israeli, na haya huyafahamu?


Mafarisayo wakawasikia makutano wakinungʼunika hivi kwa khabari zake: bassi Mafarisayo na makuhani wakuu wakatuma watumishi illi wamkamate.


Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati,


Pakawa makelele mengi. Waandishi wa upande wa Mafarisayo wakasimama, wakamtetea, wakisema, Hatuoni uovu wo wote katika mtu huyu; bali ikiwa roho au malaika amesema nae tusishindane na Mungu.


Hatta assubuhi wakubwa na wazee na waandishi wakakusanyika Yerusalemi,


Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi: wakaniwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo