Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 2:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki Yahudi mahali pa Herode baba yake, akaogopa kwenda huko; akaonywa katika ndoto, akaenda zake hatta pande za Galilaya,

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao, mwanawe Herode, alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye, baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda pande za Galilaya,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao, mwanawe Herode, alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye, baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda pande za Galilaya,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao, mwanawe Herode, alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye, baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda pande za Galilaya,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Lakini aliposikia kwamba Arkelao alikuwa anatawala huko Yudea baada ya Herode baba yake, aliogopa kwenda huko. Kwa kuwa alikuwa ameonywa katika ndoto, akaenda zake sehemu za Galilaya,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Lakini aliposikia kwamba Arkelao alikuwa anatawala huko Uyahudi mahali pa Herode baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye akiisha kuonywa katika ndoto, akaenda zake sehemu za Galilaya,

Tazama sura Nakili

Mathayo 2:22
18 Marejeleo ya Msalaba  

Alipokuwa akifikiri haya, malaika wa Bwana akamtokea katika udoto, akisema, Yusuf, mwana wa Daud, usikhofu kumchukua Mariamu mke wako, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

ALIPOZALIWA Yesu katika Bethlehemu ya Yahudi zamani za mfalme Herode, majusi wa mashariki walifika Yerusalemi,

Hatta alipofariki Herode, malaika wa Bwana akamtokea Yusuf katika ndoto huko Misri, akinena,

Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake, akatika inchi ya Israeli.

Ndipo Yesu akafika hatta Yordani kwa Yohana kutoka Galilaya illi abatizwe nae.

Nao walipokwisha kuyatimiza yote yaliyomo katika sharia ya Bwana, wakarudi Galilaya hatta mji wao Nazareti,

Wakajibu, wakamwambia, Wewe nawe umetoka Galilaya? Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo