Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 2:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Na hawo walipokwisha kwenda zao, malaika wu Bwami akamtokea Yusuf katika ndoto, akiuena, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukakae huko mpaka nikuambiapo; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Baada ya wale wageni kuondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto, akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapokuambia, maana Herode anakusudia kumuua huyu mtoto.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Baada ya wale wageni kuondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto, akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapokuambia, maana Herode anakusudia kumuua huyu mtoto.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Baada ya wale wageni kuondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto, akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapokuambia, maana Herode anakusudia kumuua huyu mtoto.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Walipokwisha kwenda zao, malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea Yusufu katika ndoto akamwambia, “Amka, umchukue mtoto na mama yake, mkimbilie Misri. Kaeni huko hadi nitakapowaambia, kwa maana Herode anataka kumtafuta huyu mtoto ili amuue.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Walipokwisha kwenda zao, malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea Yusufu katika ndoto, akamwambia, “Ondoka, mchukue mtoto na mama yake mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapowaambia, kwa maana Herode anataka kumtafuta huyu mtoto ili amuue.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 2:13
29 Marejeleo ya Msalaba  

Alipokuwa akifikiri haya, malaika wa Bwana akamtokea katika udoto, akisema, Yusuf, mwana wa Daud, usikhofu kumchukua Mariamu mke wako, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.


Watakapowaudhi katika mji huu, kimbilieni mwingine: kwa maana ni kweli nawaambieni, Hamtaimaliza miji yote ya Israeli, hatta ajapo Mwana wa Adamu.


Nao wakiisha kuonywa katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.


Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake hatta Misri;


Bassi Herode, akiona ya kuwa amedhihakiwa na majusi, akaghadhabika sana, akatuma watu kuwaua watoto wote wanawaume waliokuwa Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wa miaka miwili na waliopungua, kwa muda aliouhakiki kwa majusi.


Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki Yahudi mahali pa Herode baba yake, akaogopa kwenda huko; akaonywa katika ndoto, akaenda zake hatta pande za Galilaya,


Wakasema, Kornelio akida, mtu mwenye haki, mcha Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, alionywa na malaika mtakatifu kutuma watu kwako, uende nyumbani kwake, apate kusikiliza maneno yako.


Na yule malaika aliyesema nae akiisha kuondoka, Kornelio akaita watumishi wawili wa nyumba yake, na askari mmoja, mtu mtawa, katika wale waliomkhudumia daima:


Hatta Petro alipofahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na kutazamia kwa taifa la Wayahudi.


Marra malaika wa Bwana akasimama karibu nae, nuru ikamulika chumbani mle, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo ikamwanguka.


Yule mlinzi wa gereza akamwarifu Paolo maneno haya ya kama, Makadhi wametuma watu kuwafungulieni! bassi, sasa tokeni nje, enendeni zenu kwa amani.


lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema,


Huyo akawafanyia hila baba zetu, na kuwatenda mabaya baba zetu, akiwaamuru watupe watoto wao wachanga, illi wasiishi.


Mwanamke yule akapewa mabawa mawili kama ya tai yule mkubwa, illi aruke, aende zake nyikani hatta mahali pake, bapo alishwapo wakati na nyakati na nussu ya wakati, mbali ya nyoka huyo.


Na mkia wake wakokota thuluth ya nyota za mbinguni na kuziangusha katika inchi.


Yule mwanamke akakimbilia nyikani ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, illi wamlishe huku siku elfu na miateen na sittini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo