Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 19:28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

28 Yesu akamwambia, Amin, nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata, katika zamani za kuzaliwa upya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Yesu akawaambia, “Nawaambieni kweli, Mwana wa Mtu atakapoketi katika kiti chake cha enzi kitukufu katika ulimwengu mpya, nyinyi mlionifuata mtaketi katika viti kumi na viwili mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Yesu akawaambia, “Nawaambieni kweli, Mwana wa Mtu atakapoketi katika kiti chake cha enzi kitukufu katika ulimwengu mpya, nyinyi mlionifuata mtaketi katika viti kumi na viwili mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Yesu akawaambia, “Nawaambieni kweli, Mwana wa Mtu atakapoketi katika kiti chake cha enzi kitukufu katika ulimwengu mpya, nyinyi mlionifuata mtaketi katika viti kumi na viwili mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Isa akawaambia, “Amin, nawaambia, wakati wa kufanywa upya vitu vyote, Mwana wa Adamu atakapoketi kwenye kiti chake kitukufu cha enzi, ninyi mlionifuata pia mtaketi katika viti kumi na viwili vya utawala, mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Isa akawaambia, “Amin, nawaambia, wakati wa kufanywa upya vitu vyote, Mwana wa Adamu atakapoketi kwenye kiti chake kitukufu cha enzi, ninyi mlionifuata pia mtaketi katika viti vya enzi kumi na viwili, mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.

Tazama sura Nakili




Mathayo 19:28
35 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.


Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata: tutapata nini bassi?


Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza hawa wanangu waketi mmoja mkono wako wa kunme; na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako.


Hatta atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja nae, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake:


Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki yake; na haya yote mtazidishiwa.


Yesu akamwambia, Mbweha wana matundu, na ndege za anga vituo; bali Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.


Wakamwambia, Utujalie sisi tuketi, mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto katika utukufu wako.


ambae ilimpasa kupokewa mbinguni hatta zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa vinywa vya manabii wake tokea mwanzo wa ulimwengu.


kama tukistahimili, tutamiliki pamoja nae pia; kama tukimkana yeye, yeye nae atatukana sisi:


Lakini, kwa sababu ya ahadi yake tunatazamia mbingu mpya na inchi mpya, ambayo haki itakaa ndani yake.


Na wale wazee ishirini na wane waketio mbele ya Mungu katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifudifudi, wakamsujudu Mungu,


NA ishara kuu ilionekana mbiuguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota thenashara.


Nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, wakapewa hukumu: nikaona roho zao waliokatwa kichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia nyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea alama yake katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; wakawa hayi, wakamiliki pamoja na Kristo miaka elfu.


Na yeye aketiye juu ya kiti cha enzi akasema, Tazama, nafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika, kwa maana haya ni maneno ya kweli, na ya uaminifu.


Kati ya njia kuu yake na ule mto, upande huu na upande huu, mti wa uzima, uzaao matunda thenashara, mwenye kutoa matunda yake killa mwezi, na majani ya mti huo ya kuwaponya mataifa.


Wala hapatakuwa usiku huko; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu awatia nuru, nao watamiliki milele hatta milele.


Yeye asbindae, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.


Na viti ishirini na vine vilikizuniguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wane, wamekeli, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu.


Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika killa kabila ya wana wa Israeli, watu mia na arubaini na nne elfu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo